December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Mstaafu Dkt. Kikwete atembelea Banda la CBE Sabasaba

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Ndugu Patroba Chaulo, (katikati) leo Julai 6, 2024 wakati alipotembelea banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 48 ya Biashara yanaoyoendelea jijini Dar es Salaam. Walio katika sare ni wanafunzi wa CBE walioshiriki Maonesho hayo.

Wadau mbalimbali waliotembelea banda la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),leo Julai 6, 2024 katika Maonesho ya 48 ya Biashara (sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam wakipatiwa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Chuo hicho.

CBE inapatikana katika banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo pamoja na kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi pia wanatoa huduma ya kusajili hapo hapo wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho.