January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Magufuli kuwapa wanawake fursa zaidi

Na Waandishi Wetu, TimesMajira Online

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli amesema kuwa ataendelea kuwaamini wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi wake.

Ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akihutubia mkutano wa kwanza wa Bunge la 12.

”Nipende kuwambia wanawake Serikali yangu itaendelea kuwaamini na kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi maana nimeona mnavyochapa kazi ndio maana hata Makamu wa Rais ni Mwanamke,”amesema Rais Magufuli.