October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Lubango Kilangi

Rais Magufuli ameteua Mwanasheria Mkuu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa kwanza katika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo Prof. Adelardus Lubango Kilangi anachukua nafasi hiyo kwa kipindi cha pili, baada ya uteuzi wa kipindi cha kwanza kumalizika tarehe 05 Novemba, 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mawasiliano Ikulu na kusambazwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amefanya uteuzi huo wa kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili kufuatia uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, 2020.

Rais Magufuli alishinda uchaguzi huo kwa kishindo huku Dr. Hussein Ali Mwinyi akishinda kwa upande wa Zanzibar na kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, akichukua nafasi iliyoachwa na Rais aliyemaliza muda wake, Dkt Ali Mohammed Shein.