Na Mwandishi wetu, Timesmajira
RAIS wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 85 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God(TAG) ambayo yatafanyika Julai 14 mwaka huu katika viwanja vya uhuru Jijini Dar es salaam.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mchungaji Dkt Barnabas Mtokambali wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilele cha Maadhimisho hayo.
Amesema dhima ya maadhimisho hayo ni kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake na kuliwezesha Kanisa hilo kubaki imara kama Taasisi kwa miaka 85.
Mchungaji Dkt Mtokambali amesema kuelekea Maadhimisho hayo wamejikita katika maeneo matatu ya kumshukuru Mungu ikiwa ni pamoja na agizo kuu, kuzaa na kulea viongozi pamoja na miradi ya maendeleo.
“Kilele cha Maadhimisho haya ni fursa adhimu ya kuungana pamoja na waumini, viongozi wa dini, viongozi wa Serikali kumshukuru Mungu na kumtukuza kwa ajili ya miaka 85″amesema Dkt Mchungaji Mtokambali
Na kuongeza kuwa
“Tunataka kuweka historia mpya ..tunataka kudhibitisha dhamira yetu ya kuendelea kuwa chanzo cha matumani, amani , upendo na mabadiliko chanya katika jamii “amesema Mchungaji Dkt Mtokambali
Aidha amesema Kanisa hilo linajivunia kuwa sehemu ya Tanzania na kuhakikisha wanaendelea kuchagia katika maendeleo ya nchi .
Pia amesema wamekusudia kufanya ibada kubwa ya kumshukuru Mungu ambapo shughuli mbalimbali zimeandaliwa zinazolenga kuwahamasisha watu kutimiza Umoja na mshikamano na kujenga mazingira ya furaha na shangwe.
“Kupitia kilele cha Maadhimisho haya tutafanya makongamano ya vijana zaidi ya elfu 10000 wenye umri wa chini ya miaka 34 nchini kote, pamoja na semina maalumu ya uongozi kwa viongozi wa ngazi za juu wa Serikali Jeshi na Polisi pamoja na mikutano mikubwa ya injili.”amesema Mchungaji Dkt Mtokambali
Pia amesema kutakuwa na semina maalumu ya viongozi wa ngazi za juu wa dini na madhehebu mbalimbali, pamoja na kutoa huduma za kijamii, ikiwemo kuwafikia watoto takribani elfu 6000 wa Shule za Msingi za Jiji la Dar es salaam sambamba na kutoa taulo za kike kwa wasichana.
Vilevile amesema wameandaa shughuli za kuchangia katika miradi ya maendeleo ya jamii kama uchimbaji visima vya maji safi katika shule za msingi Jijini Dar sa salaam .
“Katika mradi wa uchimbaji wa visima vya maji tunaunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kumtua mama ndio kichwani kwa kumuondolea mtoto kero za maji kichwani”amesema Mchungaji Dkt Mtokambali
Aidha aliiushukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan katika miaka 85 ya kuwepo kwa kanisa hilo kwa kutengeneza mazingira rafiki yaliowezesha Kanisa hilo kutekeleza majukumu yake kwa uhuru .
“Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kutupatia misamaha ya kodi kwa ajili ya vifaa vyetu vya Kanisa kila mara .. tunaendelea kumuomba Mungu awalinde viongozi wetu”amesema Mchungaji Dkt Mtokambali.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba