December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt Samia atajwa kiongozi mwenye kupigania haki

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC)Ndele Mwaselela amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye upendo mkubwa kwa watu wake, na ndiye Rais namba moja kwa duniani kwa kupigania na kutetea haki za watanzania .

Mwaselela amesema hayo Mei 28,2024 wakati akiwa mgeni rasmi kwenye mkutano maalumu wa machifu zaidi ya 200 kutoka tarafa tatu za Halmashauri ya Mbeya Vijijini wa kupanga mipango mbalimbali ya kujiandaa na tamasha la ngoma za asili ambalo litafanyika siku za hivi karibuni katika mji mdogo wa Mbalizi.

Amesema kuwa Rais Samia amekuwa kiungo muhimu kwa watanzania kwa kuwaunganisha na pamoja na kupigania na kutetea haki za watanzania .

Hata hivyo MNEC Mwaselela ameomba machifu kuendelea kuunga mkono mazuri yote ambayo yanatekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Hassan Suluhu ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Machifu wangu nipende kuwaeleza kuwa Rais Dokta Samia Hassan Suluhu anawapenda sana Machifu, niwahakikishie msiwe na wasiwasi wowote anawatambua na ndiyo maana ni chifu mwenzenu, anaitwa Chifu Hangaya yote hayo ni kutambua mchango wenu katika jamii, endeleeni kumuumga mkono Mheshimiwa Rais” Mwaselela

Hata hivyo kupitia mkutano huo pia M-NEC Mwaselela amewachangia Machifu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni tano (5,000,000) ili kuwaunga mkono katika shughuli mbalimbali za kutumikia jamii, ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa mazingira.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Machifu wa Mbeya Vijijini ,Shayo Soja, amesema machifu bado wana nafasi kubwa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea kwa jamii, hivyo Serikali haina budi kuendelea kushikamana na kundi hilo katika kudumisha mira na desturi za taifa.

Chifu Masoko ameleza kuwa lengo la kuandaa mkutano huo, kwanza ni kuwaleta pamoja machifu wa tarafa zote tatu za Mbeya Vijijini, pili kupanga mikakati mbalimbali ya kufanikisha tamasha lao la kijadi ambalo limepangwa kufanyika mji mdogo wa Mbalizi mapema mwaka huu.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini Akimu Mwalupindi amemshukuru MNEC Mwaselela kwa mchango huo wa Machifu kwani kwa kufanya hivyo anasaidia kuendele kukijenga chama cha mapinduzi ndani ya wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.