January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt. Samia aridhishwa na mradi wa kuzalisha mbegu za mazao

Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo ametembelea mradi wa umwagiliaji unaotekelezwa na serikali katika shamba la kuzalisha mbegu Kilimi lililopo Wilayani Nzega na kutaka usimamiwè ipasavyo.

Amesema mradi huo ni muhimu sana, kama utasimamiwa ipasavyo utaipunguzià serikali gharama za kuagiza mbegu nje ya nchi.

Amemtaka Wakala wà mbegu nchini (ASA) kuharakisha mradi huo ili kuongeza uzalishaji wa mbegu kwa ajili ya wakulima.

Ameagiza Wafanyakazi na Bodi nzima ya ASA kusimamia ipasavyo shamba hilo ili kutimiza azma ya serikali ya kuzalisha mbègu za kutosha kwa ajili ya wananchi.

Rais amesisitiza kuwa azma ya serikali ifikapo mwaka 2030 ni kuwa na kilimo chenye utoshelevu wote na tija kubwa kwa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Aidha amewataka kuhakikisha mbegu zinazozalishwa zinawafikia wakulima kwa wakati na kwa bei nafuu.

‘Serikali itaendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo, nataka fedha zote zinazotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo kutumikà ipasavyo’, amesema.

Ili kuinuà zaidi sekta hiyo amewatàka vijana na jamii kwa ujumla kuchangamkia fursa ya kilimo ili kunufaika zaidi, huku akiahidi kuwa serikali yake itaendelea kuwasaidia ikiwemo kuwapelekea mbolea ya ruzuku.

Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Hussein Bashe ameishukuru serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipa kipaumbele kikubwa sekta hiyo.

Amesema mradi huo wa umwagiliaji unatekelezwa kwa gharàma ya zaidi ya sh bil 6 na sasa umefikia asilimia 75.

Amebainisha kuwa utàkapokamilika utaongeza kwà kiasi kikubwa uzalishaji wa mbegu za mazao mbàlimbali nçhini.

‘Mheshimiwa Rais kwa kutambua na kuthamini jitihada zako za kuboresha sekta ya kilimo nchini tumeamua shamba hili Liitwe SAMIA BLOCK FARM,’ amebainisha.

Bashe amebainisha baadhi ya mbegu zitakazozalishwa katika shamba hilo kuwa ni mahindi, mpunga, alizeti, choroko, mtama na jamii ya kunde.

Naye Mtendaji Mkuu wa ASA, Dkt Sophia Kashengè àmesema uwekezaji wa mradi huo utawezesha Wakala kuzalisha mbegu kwa mwaka mzima kupitia teknolojià hiyo ya umwagiliaji hivyo kuwezesha wakulima wengi kunufaika.

Amefafanua kuwa awali asilimia 70 ya mbegu zote zinazotumiwa na wakulima zinazalishwa nje ya nchi.

Dkt Sophia ameongeza kuwa kwa sasa kuna jumla ya mashamba 16 ya uzalishaji mbegu katika Mikoa 12 lakini hayatoshelezi, hivyo akabainisha kuwa dhamira yao ni kuongeza mashamba ya umwagiliaji ili kutosheleza mahitaji ya wakulima, mahitaji ya ASÀ ni kuzalisha tani laki 3 hadi 6 za mbegu.

Miundombinu ya Umwagiliaji katika Shamba la Mbegu lililopo Kilimi, Nzega Mkoani Tabora tarehe 18 Oktoba, 2023.
Taswira ya Chanzo cha maji katika Skimu ya umwagiliaji Kilimi, Nzega Mkoani Tabora tarehe 18 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati wakitoka kukagua chanzo cha Maji katika Shamba la Mbegu Kilimi, Nzega Mkoani Tabora tarehe 18 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya umwagiliaji katika Shamba la Mbegu Kilimi, Nzega Mkoani Tabora tarehe 18 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya umwagiliaji katika Shamba la Mbegu Kilimi, Nzega Mkoani Tabora tarehe 18 Oktoba, 2023.