Na Nwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Brandenburg jijini Berlin, Ujerumani na kupokewa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dkt. Abdallah saleh Possi.
Rais Dk. Mwinyi ameambatana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Mwita, Naibu Waziri wa Mambo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu (Special Olympics World Games) ambayo maelfu ya wanamichezo wenye mahitaji maalumu kushindana katika michezo mbalimbali, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe: 17 hadi 25 Juni 2023.
Mbali na kushiriki uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu jijini Berlin, Rais Dk, Mwinyi pia atakutana na viongozi wa juu wa Serikali nchini humo, Wakuu wa Mashirika mbalimbali, Wawekezaji na jamii ya Watanzania waishio Ujerumani (Diaspora).
More Stories
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu
Jeshi la Polisi Katavi laanika mafanikio 2024