RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa Uchaguzi Mkuu Ujao Utafanyika kwa Amani na Utulivu.
Alhaj Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipotoa Salamu baada ya Kujumuika kwa Sala ya Ijumaa Masjid Raudha Uliopo Darajabovu, Wilaya ya Mjini.
Amefahamisha kuwa Dhamira ya Serikali anayoiongoza ni kuona Uchaguzi huo kuwa ni Kielelezo cha kuwepo kwa Amani ya kudumu hapa Nchini na kila Mwananchi anapata fursa ya kutekeleza haki ya Msingi ya Kikatiba ya kupiga Kura.
Alhaj Dkt.Mwinyi amesema ni Wajibu wa Msingi wa kila Mwananchi Kuhakikisha Amani iliopo inadumishwa wakati huu na Baada ya Uchaguzi Ili Nchi ipige hatua zaidi za Maendeleo katika Nyanja tofauti.
Aidha amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu Kuendeleza utaratibu wa Kuwasaidia Watu wanaohitaji Misaada kama ilivyofanyika vema wakati wa Mwezi wa Ramadhani.
Dkt.Mwinyi ameeeleza kuwa Mwenendo Mzuri uliotekelezwa wakati wa Ramadhani unapaswa kuendelezwa kwa kiwango kile kile kwani bado makundi ya Wanaohitaji Kusaidiwa yapo ndani ya Jamii.
Naye Katibu Mtendaji wa Afisi ya Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume amewahimiza Waumini hao Umuhimu wa Kumuombea Dua Kiongozi wa Nchi kuwa ni Wajibu wa kila Muumini wa Kiislamu kwani kutengemaa kwa Kiongozi ndio nyenzo Muhimu na dira ya Mafanikio ya Taifa .







More Stories
Waziri Mkenda aeleza Tanzania ilivyoweka mikakati madhubuti Teknolojia ya Akili Unde
Polisi Mbeya yajivunia miaka minne ya mafanikio
Wahariri wa vyombo vya habari nchini wapongezwa