November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt.Mwinyi akoshwa na mdahalo wa Wanawake na Muungano,aipongeza UWT

Na Mwandishi wetu, timesmajira

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi kubwa waliyoifanya kuwaletea maendeleo wanawake na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kuandaa mdahalo wa wanawake na Muungano.

Pia, ameupongeza umoja huo kwa kuendelea kuwa kinara katika kubuni na kutengeneza mambo mbalimbali yenye lengo la kuimarisha CCM, kikiunganisha na wananchi na kuimarisha umoja na mshikamano na wananchi.

Dkt. Mwinyi amesema hayo jijini Dar es Salaam leo Aprili 25, 2024 alipofungua mdahalo wa kitaifa wa Wanawake na Muungano uliondaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City.

Mdahalo huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wake za viongozi wakuu wastaafu, mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wawakilishi, wananchi na wanachama wa jumuiya hiyo na wa CCM.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT Taifa ,Mary Pius Chatanda amesema wanafanya mdahalo wa kuelekea miaka 60 ya Muungano na kujadili nafasi ya mwanamke katika kipindi cha nyuma,sasa na kijacho

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa UWT, Zainab Shomari amesema muungano huo uliletwa na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar zikiwa huru, haukuwa wa kuchanganya mchanga tu, bali wa kidamu kwa kuwa Zanzibar kuna watu wa makabila mbalimbali.