Na Haji Mtumwa, TimesMajira Online, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewashukuru wananchi wenye uwezo mbao wamejitolea kuwasaidia wananchi maskini na wale wanaoishi katika mazingira magumu katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Alhaj Dk. Mwinyi ametoa shukurani hizo kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja, ambapo kwa nyakati tofauti alikabidhi sadaka za chakula kwa wananchi wa makundi tofauti hao katika eneo la TC Dunga Wilaya Kati pamoja na Unguja Ukuu kwa wanachi wa Wilaya ya Kusini Unguja.Â
Amesema ni jambo jema kwa wananchi hao kuwasaidia watu wengine wenye uwezo duni, huku akiwataka wananchi hao kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuwaombea dua.
Alhaj Dk. Mwinyi aliwataka wananchi hao kulitumia vyema kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani, kwa kuzidisha kufanya ibada na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa pamoja na kuitafuta Lailatul Kadr.
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hadidi Rashid Hadidi alimueleza Alhaj Dk. Mwinyi kuwa wananchi wa Mkoa huo wamefarijika sana na sadaka hiyo.
Miongoni mwa sadaka hizo zilizokabidhiwa kwa jamii ya watu wenye ulemavu, mayatima pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu ni pamoja na mchele, sukari, unga, ngano, mafutayakupikia pamoja na tende.
Katika hatua nyengine, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Mwiyi alishiriki katika hafla ya Futari aliiyoiandaa kwa ajili ya wananchi wa Mkoa huo iliofanyika katika Ukumbi wa Dk. Ali Mohammed SheinTunguu, Mkoa Kusini Unguja.
Katika salamu zake, Alhaj Dk. Mwinyi aliahidi kuendeleza utamaduni wa kufutarisha kila mwaka kama alivyorithi kutoka kwa watangulizi wake.
Nae, Mkuu wa Mkoa huo Hadidi Rashid Hadidi ,alimshukuru Alhaj Dk. Mwinyi kwa maandalizi ya futari hiyo na kusema wananchi wa Mkoa huo wamefarijika sana.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda