January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dk. Samia asisitiza Watanzania kulipa kodi

Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAIS Samia Suluhu Hassan,amwsisitiza Watanzania kulipa amesisitiza hilo akiwa
akiwa njiani kuelekea Dodoma baada ya kumaliza ziara yake mkoani Rukwa

Dkt Samia alisema inayotekelezwa inatokana
na pesa inayoikusanywa kwa njia ya kodi.

“Niwaombe pamoja ndugu zangu wafanyabiashara popote pale ulipo lipa unachokilipa ili tujenge Taifa letu,” alisema.

Wakati huo hip, Rais Samia amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo asimamie shughuli zote za matibabu ya mtoto mwenye ulemavu wa mguu aliyejitokeza katika mkutano wa njiani wakati akiwasalimia Wananchi wa Tunduma akielekea Dodoma Mara baada ya Kumaliza Ziara yake Mkoani Rukwa juzi.

Rais Samia alisema gharama zote za matibabu kumhusu mtoto huyo zitakua chini ya ofisi yake na kama kutakua na hoja yakuletwa Dar es salaam basi apelekwe haraka kwa ajili ya hayo matibabu.

Aidha, Rajis amemuondolea gharama zote za matibabu Mama aliyejitokeza katika mkutano wake wa njiani uliofanyika jana wakati akiwasalimia wananchi wa Mlowo Wilaya Mbozi Mkoa Songwe Njiani kuelekea Dodoma

Rais amemuagiza Naibu wa waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel ahakikishe Mama huyo aliyesema mtoto wake ana tundu la moyo pia Mirija yakusafirisha damu safi na salama imeungana huku gharama za matibabu ikiwa ni milioni nane laki nane na elfu hamsini atibiwe haraka

“Mtoto atibiwe Kadri kadri tutakavyoweza ,ninachotaka mtoto atibiwe ,” alisema Dkt Samia.

Alisema Serikali imejenga Hospitali maeneo yote pamoja na Rufaa ,Sasa Hospitali hizi ndani ya mikoa ni Hospitali za Kisasa na lengo ni kuzuia Watanzania kupelekwa nje kwa matibabu labda tatizo liwe kubwa sana tumelishindwa”

Rais samia aliongeza kuwa Serikali imejenga Hospitali kwa gharama kubwa na kisasa ili kuzuia Watanzania kwenda nje ya Nchi .

Alisema hospitali hizo kutoka ngazi za wilaya kwenda Rufaa , matibabu hayo yanagharama kwaio Watanzania lazima wachangie huduma za afya kwa kukata Bima za afya