Na Penina Malundo,Timesmajira
KATIBU wa NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdalla Hamid, amesema safari za kikazi nje ya nchi anazozifanya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, zina tija kwa taifa.
Amesema hayo leo Julai 28, 2024, katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi, mkoani Mtwara.
Rabia amesema, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akijenga mahusiano mazuri na mataifa mengine, huku akishawishi uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na kilimo.
Ameongezea kuwa zipo kampuni za nje zikiwemo za Uholanzi, zimewekeza kwenye viwanda vya kubangua korosho na kupandisha kiwango cha ubanguaji kutoka tani 5000 kwa miaka mitatu iliyopita hadi zaidi ya tani 20,000 kwa sasa.
Aidha ametaja kuwa juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuunganisha nchi zinazolima zao la korosho Afrika kuwa na sauti moja katika zao hilo, zinalenga kuchochea na kuongeza bei ya korosho kwa manufaa ya wakulima wa zao hilo wakiwemo wa Mtwara
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best