November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rabia,Ochola wateta shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Common Wealth London

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Katibu wa NEC Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdalla Hamid amefanya mazungumzo na Shem Ochola, Naibu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Common wealth Foundation ambaye aliambatana na Sheila Ruiz, Meneja wa Uhamasishaji na Ubunifu kutoka katika taasisi hiyo.

Katika Mazungumzo hayo Ochola na Sheila Ruiz wamemueleza,Rabia shughuli mbalimbali zinazofanya na Taasisi ya Commonwealth Foundation ikiwemo ni pamoja na kuhamasisha masuala ya utunzaji wa mazingira, Uboreshaji wa huduma za afya, kukuza demokrasia, uwajibikaji, usawa wa kijinsia, na haki za binadamu.

Kwa Tanzania taasisi hiyo kupitia asasi za kiraia inafadhili miradi mbalimbali inayowasaidia wakulima wadogo wadogo kuboresha uzalishaji kwa kutumia mbinu za kilimo kinacholinda mazingira na matumizi ya teknolojia bora zinazopunguza uharibifu wa ardhi na misitu.

Kwa upande wa utunzaji wa mazigira taasisis hiyo inafadhili baadhi ya asasi za kirai zilizojikita katika utunzaji wa vyanzo vya maji, upandaji wa miti, na juhudi za kukabiliana na uharibifu wa misitu ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, kusaidia kuhifadhi bayoanuwai, na kuimarisha juhudi za upunguzaji wa hewa ukaa
Kwa upande wake, Rabia amelezea juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na CCM chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amefafanua kuhusu falsafa ya Rais Samia ya 4R , yaani Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reforms (Mabadiliko), na Rebuilding (Ujenzi upya) jinsi zilizosaidi kuimarisha umoja wa kitaifa na kuwaunganisha Watanzania .

Aidha ameelezea hatua zinazochukuliwa na serikali inayongozwa na CCM katika masuala ya utunzaji wa mazingira.

Amewajulisha kuwa suala la uhifadhi wa mazingira ni suala linalopewa kipaumbele cha pekee na Rais Mwenyewe na katika kuhakikisha Tanzania inatokomeza ukatajiwa wa miti kwa ajili ya nishati ya kupikia, Rais amekuwa ni kinara wa kampeni ya Clean Cooking barani Afrika yenye lengo kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa ili kuhifadhi mazingira.

Rabia amesema kwamba serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuboresha huduma za afya, elimu, pamoja na kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi.

Pia amesisitiza juhudi za serikali katika kuimarisha masuala ya usawa wa kijinsia, kuhakikisha fursa sawa kwa watu wote bila kujali jinsia au umri.

Rabia ameihakikishia taasisi hiyo kuwa serikali inyaongozwa na CCM itandelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa katika masuala ya maendelea na mambo mengine muhimu yenye manufaa kwa pande zote mbili.