January 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PSSSF yachangia Timu za Taifa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akikabidhi jezi hiyo, kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (watatu kushoto) na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF, James Mlowe. (Na Mpigapicha Wetu)

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeungana na wadau wa michezo nchini, kuchangia timu za taifa za Tanzania zinazoshiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Taifa Stars, ambayo inashiriki michuano ya AFCON 2023, inayotarajiwa kuanza Januari 13, 2024 nchini Ivory Coast.

Katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya timu hizo, iliyoongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, kwenye hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Januari 11, 2024, PSSSF imenunua kupitia mnada, jezi ya marehemu Joel Bendera kwa shilingi milioni 11.

Marehemu Bendera alikuwa kocha mzalendo wa kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki AFCON kwa mara ya kwanza mwaka 1980.

Pichani, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), akikabidhi jezi hiyo, kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (watatu kushoto) na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF, James Mlowe.