Na Joyce Kasiki,Dodoma
MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa Bodi hiyo imekuwa ikichukua hatua katika madhaifu ambayo yanaweza kuleta hasara kwa serikali na kuathiri Miradi mikubwa kwa wakuu wa vitengo vya Ununuzi na Ugavi na kwamba katika mwaka wa fedha Bodi imeshachukua hatua kwa kuwaondoa kwenye nafasi zao wakuu wa vitengo 20.
Mbanyi ameyasema hayo leo Januari 19,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuhusu ya matokeo ya mitihani ya 25 ya Bodi hiyo.
“Ni kweli kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya wanunuzi na sisi kama Bodi katika mwaka wa fedhya wa 2021/22 iliamuru Wakuu wa vitengo 20 kuondolewa kwenye nafasi zao baada ya kutathimini taarifa ya matumizi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).”amesema na kuongeza kuwa
“Na tayari tumeshatuma barua 73 kuwaeleza makosa waliyoyafanya,udhaifu na makosa yaliyoonekana kwenye maunuzi na wanunuzi 68 kupeleka utetezi wao katika Ofisi ya Bodi.”
Kuhusu matokeo ya Bodi hyiyo amesema, jumla ya watahiniwa 1,216 walisajiliwa kufanya mitihani ambapo watahiniwa 1,135 sawa na asilimia 93.3 walifanya mitihani hiyo na kwamba kumekuwa na ongezeko la watahiniwa 1,031, ikilinganishwa na msimu uliopita.
“Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 452 ni wapya na waliobaki 683 ni watahiniwa waliokuwa wanarudia baadhi ya masomo,” amesema Mkurugenzi huyo.
Mbanyi ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa 613 sawa na asilimia 54.0 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 474 sawa na asilimia 41.8 watarudia baadhi ya masomo kuanzia moja hadi masomo matatu kutegemeana na idadi ya masomo aliyofeli na watahiniwa 48 sawa na asilimia 4.2 wamefeli masomo yote katika ngazi mbalimbali.
“Katika masomo 34 waliyopimwa watahiniwa, masomo 18 yalifanywa vizuri, masomo 10 yalifanywa kwa wastani na matokeo ya masomo 6 yalikuwa mabaya kwa maana ya kuwa chini ya wastani. Huku watahiniwa watatu wakiibuka kama watahiniwa bora katika ngazi za mitihani za Professional I,iii na CPSP,” amesisitiza Mbanyi
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato