Na Joyce Kasiki,TimesMajira Online,Dodoma
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako amesema atahakikisha anafanya kazi kwa bidii kutokana na imani aliyoaminiwa na Rais John Magufuli na kumrudisha kipindi kingine kuwa Waziri katika wizara hiyo.
Akizungumza jijini hapa jana alipotembelea ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba amesema licha ya kwamba amerudi katika wizara hiyo lakini sasa ni mpya maana amerudi kivingine katika utekelezaji wa majukumu yake .
“Namshukuru mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuniamini na kuniteua tena kuwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia ,alipoteua baraza lake sikufurahia sana,nikaona ni changamoto kwa sababu kuaminiwa tena kwa mara ya pili inabidi na wewe uonyeshe ilani tena kwa kufanya kazi kwa bidii zaidi,Kwa hiyo ninyi mnaweza mkaona kwamba Ndalichako ni yule yule amerudi lakini Mimi nimekuja kwa mtazamo tofauti,naangalia Mimi ni nani mpaka niendelee kuaminika kwa hiyo ninaanza upya msije mkaona tunaendelea tulipokuwa” amesema Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa
“Ilani yetu ni mpya kwa hiyo ni lazima tuwe na mipango thabiti ya kuitekeleza ili wananchi waendelee kutuamini zaidi.
Naibu Waziri wa wizara hiyo Kipanga Juma Omary ameomba ushirikiano kutoka kwa watumishi wa wizara hiyo ili kwa pamoja waweze kufanya kazi na kuhakikisha sekta ya Elimu inafanya vizuri.
Aidha amewataka watumishi hao wabadilike na waache kufanya kazi kwa mazoea .
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi