April 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Muhongo aeleza mikakati kuwapata Wataalamu wa STI

Fresha Kinasa TimesMajira Online Mara.

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof.Sospeter Muhongo amebainisha kuwa  Mahitaji makubwa ya sasa ya Dunia ni kuongeza wataalamu kwenye nyanja za sayansi,teknolojia na ubunifu (science, technology and innovation, STI) kama nyenzo muhimu  katika kuchangia kukuza maendeleo.

Ameyasema hayo Aprili 8, 2025 kupitia taarifa yake aliyoitoa ikielezea mikakati madhubuti ya Jimbo hilo linavyoendelea kujidhatiti kutekeleza miradi  itakayosaidia kuwapata Wataalamu kwenye nyanja hizo ambao watakuwa tegemeo kwa Jamii na taifa pia kwa siku za usoni.

Ambapo amesisitiza kuwa,msingi mkuu wa wataalamu wa aina hiyo ni masomo ya sayansi kuanzia shule za awali hadi kidato cha sita. Huku akiwaomba wadau na wapenda maendeleo kujitokeza kuchangia ujenzi wa maabara hizo za Masomo ya Sayansi jimboni humo.

Amebainisha kuwa, Jimbo hilo limejidhatiti”kila sekondari iliyoko Jimboni humo inakuwa na maabara tatu za masomo ya fizikia, kemia na baiolojia (sekondari zote za Kata & Binafsi) pamoja na kuongeza idadi ya “high schools” za masomo ya sayansi. 

Idadi ya “high schools” Jimboni humo   ni pamoja na  Kasoma High School katika Kata ya Nyamrandirira Tahasusi za  HKL, HGL na HGK. Suguti High School katika Kata ya Suguti itafunguliwa Julai 2025,Tahasusi za PCM, PCB na  CBG. Mugango High School Kata ya Mugango Itafunguliwa Julai 2025 ,Tahasusi za CBG na EGM.

Amesema, matayarisho ya “high schools” nyingine yanaendelea yakihusisha Mtiro High School Kata ya Bukumi vilivyopo ni bweni, umeme na maji ya bomba wanakamilisha maabara tatu za masomo ya sayansi.

Makojo High School Kata ya Makojo
Vilivyopo ni maabara mbili, maji ya bomba na umeme wanakamilisha maabara moja iliyosalia na wanajenga bweni, kwa Shilingi mil. 130 (EP4R).Bugwema High School Kata ya Bugwema vilivyopo ni maabara tatu, umeme wanasubiri maji ya bomba, mradi upo na watajenga  bweni.

“Tunayo  Kiriba High School Kata ya Kiriba Vilivyopo ni  maabara tatu, umeme, yunakamilisha  bweni,Tunasubiri maji ya bomba, mradi upo. Tunayo Nyakatende High School katika Kata ya Nyakatende Vilivyopo ni  maabara tatu, umeme na vyumba ziada vya madarasa Tutajenga bweni.Tunasubiri maji ya bomba, mradi upo. 

Matayarisho mengine ni Etaro High School Kata ya Etaro Vilivyopo ni  maabara mbili, chumba chenye kompyuta 25 na  umeme Wanakamilisha maabara moja iliyosalia wanajenga bweni huku wakisubiri maji ya bomba,mradi upo. 

Amesema,wachangiaji wa ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari  Jimboni humo ni Serikali Kuu, Halmashauri ya Musoma,Wanavijiji,Viongozi wao,  Mbunge wa Jimbo,Mfuko wa Jimbo na  Wamiliki wa sekondari za binafsi.

Kwa upande wao Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini akiwemo Shadrack Bwire wameshukuru juhudi zinazoendelea kufanywa na Mbunge wao kuhakikisha Jimbo hilo linaandaa Wasomi wengi Wana-Sayansi ambao watakuwa tegemeo kwa Jamii na Taifa katika kuleta maendeleo.

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha: Mfano wa Maabara za masomo ya sayansi zinazojengwa kwenye sekondari za Jimboni mwetu. Hiyo ni Maabara ya Kemia ya Kigera Sekondari, Kata ya Nyakatende