Na Mwandisho Wetu,TimesMajira Online
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof.kitila Mkumbo amewataka waandaji wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya 45 saba saba , pamoja na washiriki kuzingatia muongozo wa wizara ya afya wa Uthibiti wa janga la korona katika kipindi chote cha maonesho hayo.

Akizungumza Mkoani Dar es Salaam ikiwa ni siku ya kwanza kuanza kwa maonesho hayo amezitaka taasisi mbalimbali na mashirika yote kushirikiana katika kufanikisha hilo.
Maonesho ya saba saba yanatarajiwa kufungiliwa rasmi Julai 5 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo mwaka huu taasisi zaidi ya 300 za umma na binafsi ,nchi saba na kampuni za kimataifa zinatarajiwa kushiriki.
More Stories
Mhandisi Mramba:Kuuza na kununua umeme ni jambo la kawaida kwa nchi
NCAA:Filamu za ‘Royal Tour’,Amaizing Tanzania zimechangia ongezeko la watalii Ngorongoro
NHIF yaeleza inavyotumia TEHAMA kudhibiti udanganyifu