May 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Ndakidemi ashauri selimundu itibiwe bure

Na Joyce Kasiki,Dodoma

MBUNGE wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameiomba Serikali kuona namna ya kutoa huduma ya matibabu bure kwa wagonjwa wa selimundu .

Akiuliza swali Bungeni jijini Dodoma Leo Mei 16,2025 Mbunge huyo amesema ,gharama za matibabu za ugonjwa huo ni kubwa na wananchi wengi hawawezi kuzimudu.

“Naioongeza Serikali inavyopambana na ugonjwa wa selinundu ,ugonjwa huu unaenea sana maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kanda ya kati na maeneo mengine nchini , na gharama za kutibu ugonjwa huu ni kubwa sana na wananchi hawawezi kumudu ,je Serikali ina Mpango gani wa kuhakikisha wananchi wanatibiwa bure .?”amehoji Prof.Ndakidemi

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godfrey Mollel alianza kwa kumpongeza Prof.Ndakidemi kwa kuwa mtetezi wa wananchi katika Jimbo la Moshi Vijijini na kwamba tangu Jimbo hilo lianzishwe haijawahi kupata mtetezi kama yeye.

“Kwanza nimjibu Mbunge Bingwa wa Moshi Vijijini ambaye tangu Jimbo hilo lianzishwe haijawahi kupata mtetezi mzuri kama Ndakidemi “amesisitiza Dkt.Mollel

Kuhusu swali la Mbunge amesema eneo la ugonjwa wa selimundu ni Moja ya eneo ambalo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amewekeza hapa nchini.

“Rais ameleta Teknolojia ambayo mgonjwa anatibiwa na anapona kabisa ambapo mpaka sasa watoto 30 wameshatibiwa na bila malipo”amesema Dkt.Mollel

Hata hivyo amesema,Nchi inapoelekea kwenye bima ya Afya kwa wote pia itakuwa sulushisho la matibabu ya ugonjwa huo.