Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Kampuni ya michezo ya kubashiri PREMIER Bet imemtangaza Issa Amani Sitondo ambaye amejishindia shilingi Milioni ishirini na moja laki nane na sabini na nane mia tano (21,878,565) kwa kubashiri na shilingi mia tano.
Mshindi huyo ametangazwa leo na Meneja masoko wa Kampuni hiyo, Eric Kirita wakati akiwatangaza wateja wengi ambao wamejishindia pesa kutoka Premier Bet wakati wakijiandaa kwa msimu mpya wa ligi za mpira wa miguu mbalimbali Duniani.
“Hii ni zawadi kubwa ambayo itabadilisha maisha maisha yake na tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio haya” amesema Kirita
Kirita amewataja washindi wengine ambao ni Shomar Amani kutoka Mbeya, aliyejishindia 3,358,470, Raymond John mshindi wa shilingi 3,652,517 kutoka mwanza, Onesmo Marcelin kutoka Dar es Salaam mshindi wa shilingi 1,627,910.
Kirita amewataka wadau wote wa michezo ya kubahatisha kubashiri kistaarabu na kwa uwajibikaji.
“Tunawahimiza wateja wetu wote pamoja na umma kwa ujumla kufuata ushauri wa kitaalamu na kutumia mbinu za kibinadamu wakati wa kubashiri, kunashiri kunapaswa kuwa burudani na siyo chanzo cha matatizo ya kifedha au kisaikolojia”
Pia Kirita amewahimiza wateja wake na jamii ya kitanzania kwa ujumla kutazama michezo ya kubashiri kama shughuli ya burudani ikiunda mazingira ambayo furaha inachukua nafasi kuu kuliko faida ya kifedha.
Kwa upande wake Mkaguzi mkuu kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Jehudi Ngoro amempongeza mshindi huyo mkubwa na kuendelea kusisitiza wachezaji hao wa kubahatisha kuwa wacheze kwa kiasi na kupanga muda wao vizuri.
Naye mshindi huyo mkubwa, Issa Sitondo amewashukuru Premier Bet kwa ushindi huo na kuahidi fedha hizo kwenda kuzipangia matumizi sahihi ili iweze kuendesha maisha yake vizuri.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato