MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma nchini (PPRA), imesema katika Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam imejipanga kuonesha watanzania shughuli za PPRA ikiwemo matumizi ya sheria mpya ya ununuzi, sheria namba 10 ya mwaka 2023, kanuni zake pamoja na matumizi ya mfumo wa ununuzi wa Umma NeST.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Tafiti, Maendeleo na Ubunifu kutoka PPRA , Mhandisi Masunya Nashon wakati akizungumza na waandishi wa habari katika katika Maonesho hayo
Amesema Sheria mpya ya ununuzi namba 10 ya mwaka 2023 tayari imeanza kazi na imelenga kutoa wigo wa upendeleo kwa wazawa.
“Sheria hii mpya hii tofauti na Sheria iliyopita imeongeza wigo wa upendeleo kwa wazawa kuanzia kifungu cha 56 mpaka cha 64 kinaongelea habari za upendeleo kwa wazawa”amesema Mhandisi Nashon
Akitaja manufaa ya sheria hiyo mpya kuwa ni pamoja na kuongeza wigo wa maendeleo kwa wazawa ambao umegawanyika katika makundi Makuu matatu ,upendeleo kwa makundi maalum yaan vijana ,wanawake,wazee na watu wenye mahitaji maalum.
“Sheria mpya inaelekeza kila taasisi nunuzi serikalini kutenga asilimia 30 ya bajeti ya kuwezesha makundi hayo kushiriki katika makundi ya Serikali,” amesema.Mhandisi Nashon
Amefafanua kuwa, Serikali imeongeza wigo ambapo kwa sasa zile zabuni zote za shilingi bilioni 50 kushuka chini ni lazima ziende kwa wazawa .
Kwa mujibu wa Mhandisi Nashon, sheria hiyo pia inatoa upendeleo kwa ununuzi wa bidhaa za ndani kwa maana ya bidhaa zinazodhalishwa ndani ikiwa ni malighafi au chochote kinachozalishwa ndani.
Mhandisi Nashon aliongeza kuwa hadi sasa taasisi nunuzi 1,147 zimeshajiandikisha kwenye mfumo mpya wa ununuzi wa kielektroniki (NeST) pamoja na wazabuni zaidi ya 22,000 kutoka katika makundi makuu matatu ambayo sheria mpya ya Mamlaka hiyo inataka yapate zabuni za serikali.
“Idadi hii ya taasisi na wazabuni wazawa waliojiandikisha kwenye mfumo inaonesha mwitikio mzuri katika matumizi ya mfumo huo mpya”amesema na kuongeza”
“Kwa hiyo ukiangalia kwa muda mchache tofauti na mfumo uliokuwepo kwa muda wa mwaka mmoja, tunaona idadi ya wazabuni waliojiandikisha ni wengi, na tunategemea kupata wazabuni wengi zaidi maana kadri tunavyopata wazabuni wengi kwenye maombi, ndivyo ushindani unavyokuwa mpana na uwazi,” amesema.
Vilevile amesema Serikali kupitia PPRA imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo kwa makundi maalum ambapo Kwa mwaka jana walikuwa na kampeni ya kuelezea fursa ambazo zipo katika ununuzi wa Umma na walipata makundi mengi ambayo yalijiandikisha na yalikuwa na vigezo vilivyokidhi kwenye taasisi nunuzi.
“Yalipoletwa kwetu tuliyathibitisha na kuweka kwenye kanzidata ya Mamlaka na mpaka Juni 30 tulikuwa na makundi 427 kutoka katika yale makundi Makuu matatu,” amesema.
Ameongeza kuwa mfumo huo umeshaanza kutumika tangu Oktoba 2023 ambapo amesema wazabuni wanaweza kujiandikisha kupitia simu Janja mahali popote.
Ameziasa taasisi nunuzi watangaze fursa hizo kwenye mfumo wa NeST wazabuni waingie kwenye mfumo ili waweze kuona hizo fursa na mchakato utaendelea kwenye mfumo na mwisho wa siku apatikane mzabuni
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato