November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PPRA, ZPPDA watiliana saini kuenzi Muungano

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MAMLAKA ya Udhibiti na  Ununuzi wa Umma  (PPRA) Bara  na Mamlaka ya Ununuzi na uondoaji wa Mali za Umma Zanzibar (ZPPDA)
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma PPRA zimetiliana saini mkataba wa makubaliano  katika utendaji wa Mamlaka hizo kwa lengo la kuleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo ,Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Eliakim Maswi amesema maeneo waliyokubaliana katika mkataba huo ni kwenye  kushirikiana kujenga uzoefu kwa Watendaji na kukuza maarifa ya kiutendaji kwa kukubalina kubadilishana utaalam katika Ununuzi wa umma

Amesema maeneo mengine ni ushirikiano  katika kuzitambua sheria, miongozo na taratibu zinazoleta tija na uwajibikaji ndani ya taasisi hizo

“Hapa bado tunamambo tunayoyafanya ambayo ni chanya kule zanzibar wana mambo wanayoyafanya ambayo ni chanya lazima tushirikiane ili kuleta tija katika taifa hili,

“Lakini tumekubaliana kubadilishana taarifa na ujuzi muhimu unahusu ununuzi wa umma na uondoshaji Mali za umma, lakini pia tumekubaliana kuhabarishana na kupeana uzoefu na kuhusishana katika fulsa za ushiriki katika majukwaa yanayohusu manunuzi ya umma,”alisema na kuongeza kuwa

“Pia tumekubaliana kupeana msaada unaohitajika kutumia rasilimali walizonazo kutoka pande zote mbili pamoja na kuimarisha kujenga uwezo wa Watendaji kwa pande zote mbili na kuwa weka pamoja. ”

Aidha amesema haya yote unafanyika katika kuenzi miaka 60 ya Muungano ambapo lengo kubwa ni kuendelea kuudumisha na kuleta upendo miongoni mwao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ZPPDA Othman Juma Othman amesema kuwa matokeo ya mashirika no hayo ni tunu ya Muungano iliyoachwa na waasisi wa Muungano kwani maono yao yamepekeea uongozi uliopo kuendelea kusisitiza taasisi pacha kuwa na mashikiano kwa kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya Watanzania.

Amesema kuwa matarajio ya serikali ya Tanzania yatapatikana kwa wingi kwani wanaposhirikiana PPRA na ZPPRD na pia italeta tija kwa Serikali

“Ilikuwa ni kona kutoka huku kwenda huku mpaka leo tunasaini makubaliano haya ,tunakila sababu ya kuwashukuru idara ya mwana sheria Mkuu wa Serikali pamoja wataalam wetu walioitayarisha kwani wamefanya kazi nzuri sana kwa kukutana mpaka kufikia hii leo,” amesema

Hii ni shamrashamra ya kuelekea maadhimisho sherehe ya miaka 60 ya Muungano

Aidha amesema  kuwa kupitia makubaliano hayo  watakuwa wanaimarisha Muungano wa Tanzania kwani hilo ni jambo kubwa na lakifahari alisema kuwa baada ya Kusini wa kwa makubaliano hayo ipo haja ya kuwa na utekelezaji ili jambo hilo liwe na muhimu.

“Hakutakuwa na muhimu wa jambo hili kama hakutakuwa na utekelezaji kusainiwa kwa mikataba hii ni jambo namba mbona na jambo la muhimu ni ufatiliaji ili kuwepo na tija.”alisema na kuongeza kuwa

“Suala la ufuatilia ni muhimu na kuangalia kila mwaka tumefikia wapi katika utekelezaji wa makubaliano haya na pale ambapo kutakuwa na kasoro basi tutakuwa tunaweza kuzitatua na kuhakikisha tunafikia hayo makubaliano,”alisema.