Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeendelea kutoa elimu kwa Umma kuhusu mjukumu, malengo pamoja na mafanikio yake kupitia Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Kupitia maonesho ya Sabasaba yanayoendelea wananchi, wazabuni, taasisi nunuzi pamoja na wadau wa sekta ya ununuzi wameendelea kupata elimu kuhusu PPAA na majukumu yake.
Mapema leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bi. Lilian Mbassy ametembelea banda la PPAA katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Bi. Mbassy amepata fursa ya kuelezewa
majukumu na malengo ya Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kutoka kwa maafisa wa Mamlaka.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato