December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PPAA yaendelea kutoa elimu maonesho ya nanenane

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeendelea kutoa elimu kwa Umma kuhusu majukumu, malengo na mafanikio ya Mamlaka hiyo hususan kuanzishwa kwa Moduli ya usimamizi wa malalamiko na rufaa kwa njia ya kieletroniki. Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nane Nane), yanayoendelea Jijini Dodoma yalianza tarehe 01 – 10 Agosti, 2024. Banda la PPAA liko katika banda kuu la Wizara ya Fedha.