December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi yatoa ufafanuzi taarifa za tishio la ugaidi

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

MSEMAJI wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Dodoma, David Misime ametolea ufafanuzi wa taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kutoka ubalozi wa Marekani ikionyesha kuwa na uwezekano wa kigaidi nchini na kwamba limeanza kufanyia kazi taarifa hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa leo Januari 26, 2023 na David Misime imesema taarifa hiyo ilisambaa jana January 25, 2023.

Aidha SACP Misime amesema kwamba pale itakapobainika uwepo wa jambo au watu wenye kutia shaka kutokana na mienendo yao taarifa zitolewe haraka ili ziweze kufanyiwa kazi.

Misime, amesema kuwa licha ya tahadhari hiyo lakini hali ya ulinzi na usalama hapa nchini ni shwari na kwamba matukio makubwa yanayoweza kuleta hofu kwa wananchi yanaendelea kudhibitiwa.