Na Stephen Noel – Mpwapwa.
Jeshi polisi la polisi Wilayani Mpwapwa limezindua mashindano ya mpira kwa lengo la kuhamasisha jamii juu ya kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia ,madawa ya kulevya na kuhamasisha jamii kuweza kuboresha taarifa zao katika daftari ya mpiga kura kuelekeawuchaguzi wa serikali za mitaa.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa polisi Wilaya hiyo SP.Azizi Mshamu amesema wameamua kuanzisha mashindano hayo ili kuweza kuwafikia vijana wengi kwa wakati mmoja kwa kutumia mpira wa miguu.
Aidha amesema kwa kutumia michezo wameweza kupata taarifa mbalimbali za kihalifu na kuzifanyia kazi.
Kwa upande wake Mratibu wa Dawati la Jinsia Katika kituo hicho, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi , Elfrida Mapunda amesema vitendo vya ukatili katika wilaya hiyo vimekuwa vikiongezeka hivyo kwa kutumia michezo watasaidia jamii kuchukua hatua za kupunguza au kuacha.
Kapteni wa Timu ya MAZAE FC Ramadhan Kubenea amesema kuwa michezo hiyo itawasaidia vijana kujumuika pamoja na kupunguza muda wa kukaa kwenye vijiwe na kupanga uhalifu.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo