Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
JESHI la polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Ntokela Kata ya Ntokela wilaya ya Rungwe ambaye ni msanii wa Sanaa ya uchoraji aitwaye Shadrack Chaula (24)kwa kosa la kumkashifu huku akichoma picha inayomuonesha Rais Dkt.Samia Suluhu.
Akizungumza na waandishi wa habari wa habari leo Julai 2 ,2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa Juni 30,2024 katika Kijiji cha Ntokela wilaya ya Rungwe ambapo mtuhumiwa alijirekodi video na kujituma katika mitandao ya kijamii ikionyesha kutamka maneno makali ya kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamanda Kuzaga amesema kuwa baada ya kufanya tukio hilo alichoma picha moto inayomuonesha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Akielezea zaidi Kamanda Kuzaga amesema kuwa baada ya kuona taarifa hiyo inasambaa mitandaoni jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lilifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kitendo hicho na kufanya mahojiano ili kujua kwanini ameanya kufanya kitendo hicho.
“Mtuhumiwa huyu amekamatwa tayari na taratibu za uchunguzi zinaendelea,jalada limeandaliwa na kufikishwa ofisi ya mashitaka ili baada ya hatua hiyo ili aweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizi kwa kitendo alichofanya kwani ni kinyume na uungana,utamaduni na maadili ya kitanzania”amesema.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa wa Mbeya ,Juma Homera kutoa muda wa masaa 24 ,kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamini Kuzaga, kumsaka na kumkamata Kijana ambaye jina lake halijafahamika mkazi Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya Kwa kosa la Kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maneno Makali na kisha kuichoma moto picha inayomuonyesha Rais Samia Suluhu Hassan.
Homera amesema Kitendo hicho kuwa si Cha kimaadili wala Uungwana na Kiko tofauti na Utamaduni halisi wa Wananchi wa Mkoani Mbeya.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best