January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi kushirikiana na wadau kuchunguza malalamiko ya wanachi kuonewa na Askari

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Jeshi la Polisi nchini limesema limeona taarifa katika baadhi ya mitaandao ya kijamii ya kijamii zikionyesha taarifa za Wananchi ambao wanalalamika kufanyiwa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria na haki za binadamu na baadhi ya Askari Polisi.

Akitoa taarifa hiyo leo disemba 21,2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishna msadizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema wananchi hao ni pamoja na Getrude Masanja anayelalamika kufanyiwa vitendo kinyume cha sheria huko Mkoani Kilimanjaro.

Pia Msemaji wa Jeshi hilo SACP Misime amesema kuwa taarifa nyingine ni ya mwananchi aliyetambulishwa kwa jina la Kalamba anayelalamika kufanyiwa vitendo kinyume cha sheria huko Mkoani Dodoma asakari.

Aidha Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi limeziona video hizo za malalamiko hayo na limeanza kuyafanyia uchunguzi mara moja wa malalamiko hayo kwa uzito mkubwa huku akiwamba wananchi kuwa watulivu kipindi hiki ambacho Jeshi hilo linafanya uchunguzi watuhuma hizo.

Ameeleza kuwa Jeshi hilo linafanya uchunguzi wakina Ili kuhakikisha haki inatendeka huku akiongeza kuwa Jeshi la Polisi litashirikisha wataalam wengine wa haki jinai kuchunguza malalamiko hayo.

SACP Misime amewaomba wananchi mwenye ushahidi kulingana na malalamiko yalivyowasilishwa na walalamikaji katika mitaandao ya kijamii asisite kujitokeza ili uchunguzi huo ukamilike mapema na hatua nyingine za kisheria zifuate.