Na Martha Fatael, TimesMajira Online, Moshi
MPANGO wa pamoja wa matumizi ya Maji baina ya halmashauri za wilaya na wadau wa maji bonde hilo ni suluhisho pekee la kuondokana na migogoro ya watumiamaji.
Aidha halmashauri za wilaya katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga ambayo inapitiwa na bonde hilo zimetakiwa kushirikiana na bonde wakati wa kupanga miradi yenye mahitaji makubwa ya Maji.
Mkurugenzi wa PBWB, Mhandisi Segule Segule amesema hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya bonde Hilo, ambapo wadau wa maji walipewa semina na ufafanuzi kuhusu matumizi ya Maji.
Amesema mpango wa pamoja utasaidi halmashauri hizo kuwa na miradi endelevu kwani pale wanapowaza kuanzisha Kilimo au ujenzi wa viwanda patakuwa na taarifa sahihi juu ya uwepo wa maji ya kutosha.
Amesema zipo baadhi ya halmashauri ama taasisi zina mipango mikubwa ya matumizi ya Maji katika kuanzisha Kilimo au Viwanda, lakini yote hayana ufanisi mzuri kama bodi haitakuwa na taarifa katika hatua za awali.
Hata hivyo mhandisi Segule ametahadharisha wadau na jamii kwa ujumla, kwamba mwaka huu kumekuwapo na uhaba wa mvua kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, hivyo kutakuwa na upungufu wa maji na kutaka yaliyopo yatunzwe.
Mapema akifunga maadhimisho hayo,mkuu wa wilaya ya Moshi, Abasi Kayanda ameitaka PBWB kuendeleza kampeni zake za kuweka mawe ya mipaka’Bicons’katika vyanzo vya maji.
Ameipongeza PBWB kwa kuweka mipaka katika vyanzo vya maji 40 kati ya vyanzo 929 vilivyopo pamoja na kupanda zaidi ya miti 62,000 katika eneo la bonde.
Naye mwenyekiti wa bodi ya PBWB, mhandisi Ruth Koya amesema wamekusudia kuhakikisha wanapunguza migogoro ya watumiamaji lakini pia kuandaa mipango ya ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhi maji
More Stories
Mhandisi Kundo agoma kuweka jiwe la msingi mradi wa maji
Tanzania Mwenyeji wa Mkutano wa nchi zinazozalisha kahawa Afrika
Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauaji wakigombania shamba