Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Januari 06, 2023, amejumuika na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, iliyofanyika Masjid Nambar, Msikiti uliopo Vikokotoni Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Katika salamu zake kwa Waumini, Mheshimiwa Alhaj Othman, amehimiza juu ya malezi bora kwa watoto ili kuweka msingi bora wa tabia njema, kwaajili ya maisha ya hapo baadae.
Amesema kuwa Mwenyezi Mungu amewafadhilisha hata watu ambao wanaomba dua ili wapate familia na watoto bora, seuze wale wanaojitahidi katika malezi mema ya kizazi chao.
Aidha amewataka wazazi na viongozi katika nyadhifa mbali mbali, kutenda haki na uadilifu ili kuinusuru jamii kukumbwa na vitendo viovu vinavyotokana na kukosekana kwa khulka njema.
Akitoa Khutba Mbili za Ibada hiyo, Imamu Sheikh Hudhaif Shatir ameeleza makemeo dhidi ya tabia ya uongo, na kwamba Waislamu inawalazimu kuwa wakweli, ili kuthibiti katika imani, kama inavyohimiza Misingi Mikuu ya Dini ya Kiislamu.
Baada ya Swala hiyo, Alhaj Othman ametoa Mkono wa Pole kwa Familia ya Bi Dawa Mboshezi Aboud (Bi Mboshezi) kufuatia kifo cha Mama yao huyo, kilichotokea juzi, nyumbani kwao hapo Vikokotoni, Sunni Manzil, Mjini Unguja.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19