December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Othman aadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman, leo Julai 31, 2022 amejumuika na Viongozi na Waumini mbalimbali wa Kiislamu, wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Husein Ali Mwinyi, katika Kongamano maalum la Kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1444 Hijria.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar, na kubeba Mada ya “Mafunzo ya Hijra kwa Waislamu”, linafanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar, Msikiti uliopo Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.