Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo ameipongeza Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kwa kuanzisha Moduli ya kuwasilisha na kushughulikia Malalamiko kwa njia ya kieletroniki.
Bi. Omolo ametoa Pongezi hizo wakati alipotembelea Banda la PPAA katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Bi. Omolo amefahamishwa majukumu na mafanikio ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu chini ya Uongozi Imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato