Na Mwandishi wetu, timesmajira
TIMU ya Soka ya Nyumbu ya Mkoani Pwani inayojiandaa na ligi daraja la Pili imetoka sare ya goli 1-1 na timu ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Chuo Cha Polisi Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Timu ya Nyumbu huo ni mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu ambapo jana ilicheza na timu ya Mashujaa ya Mkoani Kigoma ambayo inashiriki ligi Kuu ya NBC Premium League ambapo pia ilitoka sare ya kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya michezo hiyo Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rajab Gwamku alisema kuwa anafurahishwa na viwango vya wachezaji wake kupitia michezo hiyo ya kujipima nguvu waliocheza.
Gwamku amesema wataendelea kucheza michezo ya kirafiki zaidi ili kuiimarisha timu yake kabla ya kuanza kwa michezo ya ligi daraja la pili kwa kipindi itakapopangwa kuchezwa ligi hiyo.
Amewaomba wanapwani kuiunga mkono timu yao ili iweze kufanya vyema kwenye ligi daraja la pili na kupanda daraja la kwanza huku malengo yakiwa ni kupanda ligi kuu ili kuuwakilisha vyema mkoa huo.
Amesema michezo yote waliocheza ilikuwa mizuri kwao kwani wao wanaenda kuboresha sehemu ambazo walikuwa hawajafuzu vizuri ili watakapoingia katika kucheza ligi waweze kupanda daraja.
“Mchezo ulikuwa mzuri timu ya Mashujaa na Polisi Fc imeweza kutupa nguvu za kucheza vizuri zaidi mbeleni katika mechi tulizocheza nazo za kirafikiki,”amesema .
Amesema katika timu zote wameweza kutoka sare hivyo inaonesha ni namna gani sasa wameanza kufuzu mchezo huo na kuwa tayari kuingia ulingoni katika kupata kuhakikisha wanapata ligi.
Kwa Upande wa Kocha wa Timu ya Mashujaa Fc ,Hussein Bunu amesema katika mechi yao ya kirafiki waliyocheza na Nyumbu ilienda vizuri kwani imewafanya kufanya mazoezi ya kwenda katika mechi zijazo na kuwa tayari katika kufanya vizuri.
“Tumecheza vizuri na tumepata mazoezi ya kufanyia kazi katika mechi zijazo zinazokuja za ligi msimu huu,”amesema.
Amesema timu ya Nyumbu kuelekea msimu wao mpya wa ligi daraja la pili timu hiyo ipo vizuri kwani wamewapa kitu ambacho wao wataenda kukifanyia kazi katika mechi zao zijazo.
More Stories
Serikali yaja na mwarobaini wa changamoto ya Kivuko Magogoni – Kigamboni
Kisarawe kukata keki ya Birthday ya Rais Samia
Wataalam wa afya wakutana kujadili ugonjwa wa Marburg