Na Penina Malundo, Timesmajira Online
KADA ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Lazaro Nyalandu,amerudi rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM leo katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho.
Nyalandu ametangazwa rasmi leo Dodoma katika mkutano huo na Rais wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Samia Suluhu Hassan.
Nyalandu ametoa shukrani zake kwa Mwenyekiti wa Chama hicho,kumpokea ,kumsamehe na kumruhusu kumrejesha katika chama hicho.
“Watanzania wameona nyota yako wamejaa na furaha,Mungu akakuongoze uwepo wangu mbele yako na mkutano huu ni kielezo tosha wewe kuungwa mkono na watanzania wote,”amesema
Aidha amesema sasa kazi iendee na Mwenyekiti Samia akaitwe heri kupitia CCM na kuongeza tabasamu katika nyuso za watanzania huku akiyaenzi yale yalioachwa na muasisi baba wa taifa.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya