Na Esther Macha, TimemajiraOnline ,Mbeya
MKUU wilaya ya Mbeya , William Ntinika amesema makusayo yote yanayokusanywa na halmashauri ya Jiji la Mbeya yanapaswa kuwa na tasfsiri ya matumizi yake na kufanya wananchi kuwa tayari kukusanya makusanyo hayo kwa bidii.
Akizungumza hayo jana wakati wa Mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mkapa uliopo Jijini hapa.
Ntinika amesema kuwa uwezo wa kukusanya wanao na ndo sababu ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeongeza jitihada na kuweka wataalam ambao watashirikiana nao kuhakikisha wanakusanya na kufanya vizuri katika Jiji la Mbeya.
“Historia inajieleza mwaka uliopita mlifanya vizuri ikampelekea Rais John Magufuli akamteua aliyekuwa Mweka hazina wa Jiji kuwa mkurugenzi hivyo naamini uwezo mnao mkubwa na mnaenda kufanya vizuri zaidi ya mwaka uliopita”amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha Makusanyo ya mapato mwaka wa fedha 2020/2021 wamepanga kukusanya Bil.71. ,mapato ya ndani ni Bil.15 zinatarajiwa kukusanywa.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka madiwani kuwa wabunifu kwenye kata zao kuwasukuma wale ambao wanatakiwa kukusanya kwa stakabadhi ili makusanyo hayo yaweze kuingia kwenye halmashauri ya Jiji la Mbeya ili kuonekana kufanya vizuri zaidi ,kila mapato yaingie kwenye stakabadhi.
“Kwenye matumizi miradi ambayo imewekwa kwenye mpango wa bajeti ikamilike tarehe 30 Juni naomba muwe wakali sana msiwe wakali wa kukamata watu fateni sheria na taratibu makusanyo yote yaende kulenga yale yaliyopitishwa kwenye baraza la madiwani “amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa upande wake Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya DorMohamed Issa ,amewataka madiwani na watendaji wa mitaa kuendelea kusimamia suala la usafi,suala la usafi liwe ni ajenda ya kudumu sio kusubiri viongozi ngazi ya Mkoa kuhimiza.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ,Mariam Mtunguja amesema kuna miradi katika Jiji hiyo haiendi vizuri kutokana na vituo vya afya viwili ambavyo ni Iyunga na Nzovwe havijafikia huduma ambayo ilikuwa inatarajiwa fedha walizopewa Jiji ndizo fedha walizopewa halmashauri zingine .
“Tuna vituo vya afya 15 katika katika Jiji la Mbeya ,kwani kituo cha Mpata wameweza kubeba Mchanga ,mawe ,cementi wamebeba vichwani lakini badso wameweza kujenga kituo kikubwa cha afya lakini Jiji bado wameshindwa kufuata mfano wa kituo cha afya Mpata,”amesema na kuoneza
“Suala la usafi katika Jiji la ,Mbeya lisiwe la mzaha lipewe kipaumbele kama ambavyo suala la mapato linavyopewa kipaumbele kwani eneo hilo likipewa umuhimu Jiji la Mbeya linaweza kuadilishwa jina na kupewe hadhi yake ya kuwa safi,”amesema
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari