January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NSSF yatwaa tuzo ya ushindi

 Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetwaa Tuzo kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NSSF imepokea cheti na tuzo hiyo kwa kutambua utendaji kazi wa hali ya juu katika Wiki ya Huduma za Fedha.

Wiki ya huduma za fedha hufanyika kila mwaka na inaratibiwa na Wizara ya Fedha ikishirikisha wadau wa masuala ya fedha nchini, ambao ni wizara na taasisi za serikali, mabenki, makampuni ya bima pamoja na wadau wengine wa  serikali na sekta binafsi.

Kwa mwaka huu, Wiki ya Huduma za Fedha imefanyika jijini Arusha na ilianza tarehe 20 na inafikia tamati tarehe 26 Novemba 2023.