Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imeutaka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)mkoa wa Mbeya kuanza kutoa elimu kwa wafanyakazi pindi wanapoajiriwa ili waweze kuelewa masuala mbalimbali wa mfuko huo.
Kauli.hiyo imetolewa Mei 21 ,2024 na Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Kayuni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wastaafu watarajiwa uliondaliwa na mfuko wa Taifa wa Hifadhi jamii (NSSF )mkoa wa Mbeya.
“Ni vema Sasa ifike mahali mfuko huu mkaanza kutoa elimu mapema mara tu mfanyakazi anapoajiriwa ili kuweza kufahamu masuala muhimu ya mfuko wenu”amesema Kayuni.
Awali Meneja wa huduma kwa wateja wa NSSF Robert Kadege amesema lengo semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wastaafu watarajiwa ili waweze kuelewa mambo mbalimbali ikiwemo suala la kikokotoo
Hata hivyo Kadege ametoa wito kwa waajiri kulipa michango ya wafanyakazi wao kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu pindi wanapostaafu.
Naye Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya Deus Jandwa amehimiza wafanyakazi kutumia mifumo ya kidijitali na kuhakikisha michango yao inawasilishwa kila mwezi katika ofisi za NSSF.
”Sasa hivi mifumo yetu imerahisishwa, unaweza ukaingia kwenye mifumo yetu kwa kutumia simu yako ukaangalia michango yako kama mwajili anakuletea”
Bi Subir Lugala mmoja wa wastafu watarajiwa ametoa rai kwa wafanyakazi ambao hawajajiunga na NSSF kujiunga ili kwa Vijana kujiunga na NSSF ili waweze kustafu kwa staha.
Kwa upande mwingine Dkt Maundi Keneth amesema semina hiyo imewatoa hofu na kujiandaa wanapoelekea kustaafu
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba