Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NRIC) inatarajia kuchimba visima zaidi ya 1,845 katika mwaka wa fedha wa 2023/24 nchi nzima kwa ajili ya kuweka mifumo ya umwagiliaji kwa lengo la kuzalisha chakula kwa tija na kuongeza usalama wa chakula hapa nchini.
Hayo yamesemwa jijini dodoma na mkurugenzi mkuu wa tume ya taifa ya umwagiliaji raymond mndolwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu na mikakati ya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2023/24.
Amesema hatua hiyo itawezesha  katika kila halmashauri hapa nchini kuwa na wakulima 150 ambao watapata mifumo ya umwagiliaji ili kila mkulima aweze kuzalisha kwenye ekari  mbili na nusu kwa kutumia mifumo hiyo ya umwagiliaji badala ya kusubiri kilimo cha mvua pekee..
“Mkakati huo tumeshauanza na tunahakikisha kwamba tunachimba visima, tunawawekea miundombinu ya umwagiliaji na wakulima hawa wanaenda kuhakikisha kwamba wanapata tija kwenye uzalishaji wao” amesema Mndolwa na kuongeza kuwa
“Uwekezaji katika eneo hili ni mkubwa sana na ni gharama’. kwahiyo suala la ukarabati kuhakikiwa kwamba miradi hii inakuwa endelevu ni muhimu sana”
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ,NRIC imeanzisha utaratibu wa kuchimba mabwawa, na kupitia mabwawa hayo wanakwenda kuyachimba ili kuvuna maji yale ambayo yanaporomoka.
Aidha amesema, kwa mwaka 2023/24 serikali imewapa bajeti ya shiling bilioni 373 ambapo fedha hiyo inakwenda kumalizia miradi mipya 25 waliyoianza, miradi 30 ya ukarabati na miradi sanifu 42.
“Tunakwenda kumalizia usanifu wa mabonde 22 yaliyopo hapa nchini na tunaanza ujenzi wake. ukubwa wa mabonde haya tutakayoyajenga ni zaidi ya ekari laki tatu na sitini na moja 3,61000 kama tulifanikisha zoezi hilo tunaweza kuongeza uzalishaji wa chakula kwa sehemu kubwa na biashara” alisema Mndolwa.
Mkurugenzi huyo ametumia nafasi hiyo kuwasihi wakulima wote nchini wajitahidi kukubali elimu wanayopewa na tume hiyo ili kuhakikisha kwamba wanachangia ada ya umwagiliaji, kwa sababu ndio ambayo ina uwezo wa kuwafanya wao kufanya ukarabati pale panahojitajika.
More Stories
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo
Maelfu kunufaika namsaada wa kisheria Katavi
Serikali yazidi kuwakosha wawekezaji wadau waipa tano