Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Meneja wa Kanda ya Kati Benki ya NMB,Janet Shango amekabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya T.Shs 24,567,000 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni madawati kwa ajili ya shule tano za msingi na Sekondari, mashuka, magodoro na vifaa vya kupimia afya (Kituo cha afya Kimamba).
Katika matukio hayo yaliyofanyika kituo cha afya Kimamba na shule ya sekondari Chanzulu viongozi mbali mbali wa Serikali, walimu, wanafunzi, Wazazi na wananchi mbali mbali walihudhuria hafla hiyo ikiwa ni sehemu ya Benki hiyo kuunga mkono jitihada za serikali kuwaletea maendeleo wananchi.
NMB ina matawi matatu ya kutoa huduma Wilayani humo.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM