Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya NMB imetambuliwa na kupokea tuzo tatu za kimataifa ambazo ni:
🏆 Benki Bora Tanzania 2023 (Kutoka Tuzo za Umahiri za EuroMoney)
🏆 Benki Bora ya Wateja Maalum (Kutoka Tuzo za Umahiri za EuroMoney)
🏆 Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara (Kutoka Tuzo za Global Banking and Finance Review)
Tuzo hizi zimetolewa na majarida ya kimataifa yenye makao makuu yake London, Uingereza – na leo Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna amezitambulisha rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya NMB.
“Hii ni mara ya 10 Benki ya NMB kutambulika kama Benki Bora nchini ndani ya miaka 11 iliyopita, ikidhihirisha ufanisi wetu wa kiutendaji, mapinduzi ya kiteknolojia na ubunifu, uongozi dhabiti, na uimara wetu katika kuleta masuluhisho yanayomgusa kila Mtanzania,” amesema Bi. Ruth Zaipuna.
“Tunawashukuru wateja wetu, wanahisa, wafanyakazi, Benki Kuu, Serikali pamoja na wadau wetu wote kwa kuendelea kutuamini na kutufanya kuwa Benki Bora nchini,” amesema.
Endelea kufurahia huduma za Benki ya NMB, kwani #HapaNdioNyumbani
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba