Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkazi wa Kizota Jijini Dodoma, Salum Jumanne Rajabu jana alikabidhiwa pikipiki yake baada ya kushinda katika promosheni ya “NMB MastaBata Kotekote’ inayohamasisha matumizi ya kadi na kuscan QR (Lipa Mkononi)Rajab alikabidhiwa pikipiki hiyo na Meneja wa NMB Tawi la Kambarage Jijini Dodoma, Emiliana Wilson ambaye alisema mshindi huyo alipatikana katika kwenye droo lililoendeshwa wiki iliyopita.
Rajabu alisema ni utaratibu wake kutumia NMB mastercard kwa ajili ya kufanya miamala na kulipia huduma mbalimbali kupitia kadi yake.
“Asante sana NMB kwa kunizawadia pikipiki hii na napenda kutumia mfumo huu wa malipo kwa sababu ni rahisi na salama zaidi, hivyo itakuwa jambo jema niseme kuwa tuendelee kutumia kadi zetu za NMB mastercard/ kuscan QR kufanya malipo,” alisema Rajabu.
Akikabidhi pikipiki hiyo, Emiliana alisema ushindi katika promosheni ni rahisi kuingia kwenye draw, siri yake ni kutumia NMB mastercard au kwa kuscan QR kila unafanya miamala yako na mpaka sasa washatoa zaidi ya Sh100 milioni kwa washindi 300.
Zawadi za kila wiki zitakuwepo ambapo jumla ya washindi 75 watanyakua pesa taslimu TZS 100,000 kila mmoja na mmoja zawadi ya Pikipiki (boxer), kwa mwezi jumla ya washindi 98 watanyakua pesa taslimu TZS 1,000,000 kila mmoja huku kila mwezi kukiwepo zawadi ya Pikipiki (Boxer) mbili. Zawadi ya droo ya mwisho ni safari ya siku nne huko Dubai kwa washindi saba na wenza wao.
Endelea kufanya malipo kwa kutumia NMB mastercard au Lipa Mkononi (mastercard QR) ujiwekee nafasi ya kushindia zawadi kibao na #NMBMastaBataKoteKote
More Stories
Wanasheria waombwa kusaidia kusimamia sheria, sera ulinzi wa taarifa
Wakinamama wajasiriamali wa Dodoma wamshukuru Rais Samia
Watumushi wasisitizwa kufanya kazi kwa weledi