December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB kugharamia Wateja 8 safari ya Dubai

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ikiwa zimesalia siku 3 tu kuelekea ‘Grand finale ‘ ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu, benki hiyo iliendesha droo ya wiki ya mwisho ya kampeni ya NMB #MastaBataKoteKote katika Manispaa ya Morogoro kwenye tawi la NMB – WamiKwenye droo za kila wiki, washindi 75 wamekuwa wakinyakua TZS 100,000 kila mmoja na wa 76 akishinda pikipiki aina ya Boxer. Hii imepelekea jumla yao katika droo zote 10 za kila wiki kuwa 760.

Thamani ya zawadi walizoshinda ni pamoja na TZS milioni 75 pesa taslimu kwa washindi 750 na TZS milioni 30 za Boxer 10. Jumla ni TZS milioni 105 na thamani ya zawadi zote za shindano hili la kuchagiza malipo kidijitali ni zaidi ya TZS milioni 300.

Kabla ya zoezi la kuwapata washindi wa mwisho 76 wa kila wiki, Meneja wa Tawi la NMB Wami, Bw Harold Lambileki, alisema droo ya kuwapata washindi wa kwenda Dubai itafanyika makao makuu ya benki hiyo wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

Meneja huyo alisema kila mteja wa NMB anayefanya miamala yake kwa kutumia NMB Mastercard na Lipa Mkononi (QR) anayo nafasi ya kushinda zawadi ya safari ya Dubai huku wanaochanja sana na kulipa zaidi kidijitali wakiwa na nafasi kubwa ya kuibuka kidedea.

Hata wewe unaweza kuibuka mshindi kwenye droo ya ‘Grand Finale’ wiki ijayo hivyo, usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastabataKotekote

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Wami, Harold Lambileki (kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki mshindi wa Pikipiki katika droo ya NMB MastaBata kotekote, Aidan Stephen Lukindo (katikati) kutokea Morogoro. Kulia ni Meneja wa Benki la NMB Tawi la Morogoro Business center, Hamis Rashid. Benki ya NMB imeshatoa Pikipiki kumi na 14 mpaka sasa zikiwa ni zawadi kwa wateja wa NMB wanaofanya malipo kupita NMB mastercard au Lipa Mkononi (QR) katika msimu huu wa MastaBata.