Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
BENKI ya NMB, imezindua rasmi Programu ya Muda wa Kati (Multicurrency Medium Term Note – MTN) yenye thamani ya
Sh. Trilioni 1, pamoja na kufungua Dirisha la Uwekezaji wa Toleo la
Kwanza la Hati Fungani ya Jamii (NMB Jamii Bond).
Katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Msajili wa H a zi n a , N e h e m i a M c h e c h u alisema Serikali inajivunia bunifu za viwango vya NMB, huku Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, akiitaja Hati Fungani hiyo kuwa ya
kwanza kwa ukubwa Kusini mwa
Jangwa la Sahara.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema benki yake inaanza kuiuza rasmi Jamii Bond kote nchini kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 27
mwaka huu, na baada ya hapo itapatikana katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kwa wanunuzi watakaoikosa katika
kipindi hicho.
“NMB Jamii Bond ni ya kipindi cha miaka mitatu, hadi Novemba 2026, ambako wawekezaji wake watapata riba ya asilimia 9.5 kwa mwaka na italipwa kwa vipindi
vinne kwa mwaka. Kiasi cha chini ni Sh. 500,000 na mnunuzi atapaswa kujaza fomu matawini na kwa Mawakala wa DSE waliopewa kibali na CMSA”
“Wanunuzi wa Hati Fungani hii ni watu wote, binafsi, mashirika, makampuni, lengo ni kukusanya Sh. Bilioni 75, lakini CMSA
imeturuhusu kufanya ongezeko (green shoe option) la Sh. Bilioni 25, kwa hiyo tunaweza kwenda hadi Sh. Bilioni 100.
“Tumeruhusiwa na CMSA kuuza Hati Fungani hii kwa shilingi za Kitanzania, lakini pia kwa Dola za Kimarekani, ambako tumepewa idhini ya mauzo ya Dola Milioni
10 na ongezeko la Dola milioni 5, hivyo kufanya mauzo ya Dola kuwa yanayoweza kufikia Milioni 15.
“ F e d h a z i t a k a z o p a t i k a n a zitatumika kutoa mikopo inayolenga matokeo chanya na endelevu katika
jamii, ikiwemo kwa ajili ya miradi ya
nishati mbadala, miradi ya kuzuia
na udhibiti wa uchafuzi mazingira, usimamizi wa maji safi na maji
taka na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.”
“Pia itakuwa ni kwa ajili ya m i k o p o y a k u w a w e z e s h a
wanawake na usawa wa kijinsia,
ya nyumba nafuu, usalama wa
chakula, huduma za afya, elimu,
vijana,” alibainisha Bi. Zaipuna
huku akizishukuru taasisi zote
zilizoshirikiana nao, zikiwemo
Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
CMSA, DSE, ABSA Tanzania
ambayo ni Mshauri Mwenza.
Kwa upande wake, Mkama
aliishukuru Ofisi ya Msajili Hazina
kwa kuzijengea taasisi za fedha
mazingira wezeshi katika kukuza
uchumi, huku akisema kuwa
mnamo Agosti 31 mwaka huu,
CMSA ilitoa idhini kwa NMB
kutoa Hati Fungani hiyo ambayo ni
sehemu ya Programu ya Muda wa
Kati yenye thamani ya Sh. Trilioni 1.
“CMSA ni Taaassi ya Serikali
yenye jukumu la kuhakikisha Hati
Fungani zinazotolewa zinakidhi
matakwa na vigezo vya kisheria,
ambapo mnamo Agosti 31, tulitoa
idhini kwa NMB kutoa Jamii Bond,
ambayo fedha zitakazopatikana
z i t a e l e ke z w a k a t i k a m i r a d i
mbalimbaili ya kijamii kwa ustawi
wa umma.”
“ Leo Septemba 25 ( jana) tunaiambia dunia kuwa NMB imekidhi matakwa ya kisheria kwa mujibu wa CMSA, Jumuiya za
Kimataifa kiasi cha kupewa idhini ya kuiingiza sokoni Jamii Bond.
“Historia inaandikwa leo, NMB imekuja na bidhaa ya hadhi ya juu,
hatujawahi kuwa na Hati Fungani ya thamani kubwa kiasi kisi hiki,
hii ni rekodi, sio tu kwa Tanzania na Afrika mashariki, bali ni kubwa
zaidi kuwahi kutolewa na taasisi yoyote iliyopo Kusini mwa Jangwa
la Sahara.
Naye Mchechu, aliwashukuru washirika wa mchakato huo,
h u s u s a n i w a s i m a m i z i B oT, CMSA na DSE kwa walichofanya
kufanikisha jambo kubwa na la kihistoria kutokea katika Sekta ya
Fedha nchini, ambacho ni kitu cha kujivunia na kujipongeza.
“Kazi nzuri inayofanywa na NMB,
inaipa Ofisi ya Msajili heshima
tukiwa ndio wasimamizi wa Sekta
ya Fedha. Sisi kama Serikali tunafurahia sana uwekez aji wetu ulioko NMB, tunajivunia na ndio ‘model’ ambayo tutaitumia
na kuiingiza katika Taasisi na Mashirika yetu, k wa sababu
tumeiona faida yake.
“Ni jambo jema sana soko linapochagizwa na viongozi imara na wabunifu kama waliopo NMB,
kwa kuwa viongozi waliolala wanalinyonya soko.
Ukiwa na benki kubwa kama hii, bunifu zinazoona mbali ndio jambo la kujivunia, hakika mmethubutu kuthibitisha uimara kwa kuzindua ‘bond’ ya Trilioni 1.”
“Menejimenti na Wafanyakazi,
chini ya Bodi ya Wakurugenzi, mnazitendea haki nafasi zenu, hasa
ukizingatia tuna mazingira sahihi, rafiki na ya kweli kukuza ustawi wa
Sekta ya Fedha yaliyowekwa na uongozi wa Rais Samia Hassan
Suluhu, ambaye amedhamiria kuleta mageuzi chanya katika Sekta hii
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best