November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB Foundation, ZASCO wazindua Mafunzo ya Wakulima wa Mwani Zanzibar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Asasi ya NMB Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya Mwani Zanzibar (ZASCO) wamezindua mafunzo endelevu kwa Wakulimwa wa Mwani Unguja na Pemba, ambapo Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar (SMZ) imeipongeza na kuitaja asasi hiyo kama mbia wa karibu, wa kimkakati na wa muda wote wa maendeleo Zanzibar.

Mafunzo hayo ya miezi mitatu kwa wakulima zaidi ya 1,300 kutoka vikundi 72 vya wakulima, yamefunguliwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban, yakiwa ni zao la makubaliano ya ushirikiano yaliosainiwa Machi mwaka huu kati ya NMB na Kampuni ya Mwani Zanzibar (ZASCO).

Akifungua mafunzo hayo, Waziri Omar alizipongeza NMB Foundation na ZASCO kwa kuyaingiza makubaliano yao katika vitendo kwa lengo la kuelimisha wakulima juu ya kilimo cha kisasa, upatikanaji mikopo nafuu ya kilimo na kuwajengea uwezo wa elimu ya fedha kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Machi mwaka huu tulikutana Dar es Salaam kusaini makubaliano haya, tunaposimama hapa leo tunaingia kwenye utekelezaji wa lile. Nawapongeza kwa sababu taasisi nyingi zinasaini makubaliano, lakini ‘perfomance’ hakuna, NMB na ZASCO mmeenda mbali zaidi katika hili.

“Mafunzo haya yanalenga kujikita katika maeneo matatu ya elimu ya fedha, elimu ya kilimo na uzalishaji na mwisho uwezeshaji wa kifedha kwa maana ya mikopo nafuu kwa wakulima wetu, mambo yatakayowaongoza kulima kwa tija, kutunza fedha zitokanazo na mazao, lakini kupata mitaji.

“Nawapongeza sana NMB kwa jitihada zenu zisizokoma katika kuunga mkono Ajenda ya Serikali ya Zanzibar ya Uchumi wa Buluu. Hakika sote ni mashahidi wa namna mnavyosaidiana nayo katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za Wazanzibar.

“Kama kuna mbia wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye ni mbia wa karibu zaidi, mbia wa kimkakati, lakini pia mbia ambaye wazungu wanamuita ‘of the all seasons,’ iwe mvua, kiangazi au masika, basi ni Benki ya NMB, imekuwa ikishirikiana na Serikali katika mazingira yoyote yale,” alisema Waziri huyo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa ZASCO, Masoud Rashid Mohammed, alisema mafunzo hayo sio tu zao.

Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaban (kulia) akisalimiana na Meneja Mkuu wa Asasi ya NMB Foundation, Nelson Karumuna (katikati) wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mafunzo kwa wakulima wa Mwani yalioratibiwa na Asasi hiyo kwa ushirikiano mkubwa wa Benki ya NMB na kampuni ya Mwani Zanzibar (ZASCO). Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa Benki ya NMB, Nsolo Mlozi.