Na Penina Malundo,Timesmajira
Mkurugenzi wa Utawala wa Kampuni ya Superdoll,Jamal Bayser amekipongeza Chuo cha Usafirishaji cha NIT kwa kufanya vizuri katika uzalishaji wa wahitimu wenye ubora katika kazi zao hususan wale wanaoenda kuajiliwa katika Kampuni mbalimbali nchini.
Pongezi hizo zimetolewa jana jijini Dar es Salaam wakati wa Kongamano la Wahitimu wa 12 wa Chuo cha NIT ambapo mambo mengine kupitia Kongamano hilo lililowakutanisha wadau mbalimbali wa Usafirishaji ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Chuo hicho,alisema wao kama wadau wa masuala ya usafirishaji wanaona utofauti uliopo sasa na wa miaka ya nyuma kwa wahitimu wa chuo hicho cha NIT.
”Tunawapongeza NIT kwamba kazi wanayoifanya ni kubwa katika sekta ya usafirishaji,Chuo kinazalisha wahitimu wengi kwenye kada mbalimbali na sisi tuliopo kwenye sekta hii tunafahamu ubora wa wanafunzi wanaotoka hapa.
”Kazi inayofanywa na NIT ni kubwa kiukweli tulipotoka ni tofauti na tulipo mabadiliko yanapoonekana ni mazuri,matumaini yetu kama wadau wa usafirishaji kwamba watafanya vizuri kadri wanavyokwenda,”amesema

Akitoa ushauri kwa Chuo hicho,Bayser amesema maeneo yote yanatakiwa kuongezewa nguvu hususan eneo la teknolojia ambalo linahitaji kuongezewa nguvu nyingi ili kuja gunduzi mbalimbali zitakazokuja kuleta matokeo chanya.
Amesema kadri siku zinavyozidi kazi kubwa inafanyika na wanafunzi ambao wanahitimu katika Chuo hicho wamekuwa wanaviwango vya juu katika kazi tofauti na miaka ya nyuma.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha NIT,Dkt.Prosper Mgaya amesema kufanyika kwa kongamano hilo ni kutokana na serikali kuwaelekeza kuwa na mahusiano ya karibu na sekta wanazozihudumia.
Amesema kupitia kongamano hilo wameweza kuwasilisha mawasilisho mbalimbali na wanafunzi kuonesha bunifu zao ambazo zimewekwa ili kuibua vipaji ya wanafunzi.
“Kupitia Kongamano hili kumekuwa na bunifu mbalimbali ambazo zimeletwa ili kuibua vipaji vya wanafunzi,Kila mwaka Chuo chetu uangalia bunifu ambazo zinaenda kujibu matatizo ya watanzania .
”Tumekuwa tukizifatilia bunifu hizo na kisha tunaziendeleza na kuwafanya wanafunzi hao kusimamiwa na walimu moja kwa moja,”amesema
Aidha amesema jukumu lao ni kuhakikisha wanamtengeneza wanafunzikuwa mahiri barabarani kwa madereva na kuhakikisha kwamba mafunzo wanaowapa kama yanakaa.

More Stories
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10