November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIC yatunukiwa cheti cha uhakiki ubora

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limeendelea kung’ara kwa kutunukiwa cheti cha uhakiki wa ubora ISO 9001.
2015 kwa namna shirika hilo linavyotoa huduma za haraka, ubora na uhakika kwa wananchi.

Ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam Dkt. Elirehema Doriye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) tumesherekea kupata cheti cha uhakiki wa ubora ISO 9001.2015 ambacho kinaonyesha namna NIC inavyotoa huduma za haraka, ubora na uhakika ikiwa ni wiki kadhaa zimepita tokea kupata cheti cha ‘Superbrand’ kwa kuonesha ubora wa NIC kwa utoaji wa huduma na chapa inayotambulika na mvuto Afrika Mashariki.

“Sisi ni sehemu ya watanzania hii ni kampuni ya wananchi na ni Mali ya watanzania kazi yetu kubwa ni kuhakikisha kwanza wanaelewa umuhimu wa bima katika maisha yao na katika maendeleo yao na namna ambavyo itawakinga kuwa na maisha bora zaidi” Dkt. Elirehema Doriye, Mkurugenzi Mtendaji NIC

“tumekutana kupongezana na kufanya tafakuri ya mafanikio ambayo tumeyapata kwa kupokea tuzo mbili ambazo tumekabidhiwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Arusha katika kikao kazi cha wakuu wa Taasisi na wenyeviti wa bodi” Dkt. Elirehema Doriye, Mkurugenzi Mtendaji NIC

Amesema tuzo ya kwanza ikiwa ni kampuni ya ambayo imefanya mabadiliko makubwa katika muda mfupi ya kiutendaji na ya kifedha kwa maana ya faida pamoja na kuboresha huduma na utendaji wa shirika, pia tuzo ya pili ni yakutoa gawio kubwa kwa mataasisi ya umma

“Bado matumizi ya bima yako chini ukilinganisha na mahitaji na changamoto ambazo Watanzania wanazipata kutokana na majanga mbalimbali ya kupoteza maisha, ulemavu na kupoteza Mali” Dkt. Elirehema Doriye, Mkurugenzi Mtendaji NIC

Pia Katika kuongeza utoaji wa Elimu zaidi kwa sababu NIC ina soko imara la bima kutokana kazi yetu ni kuelemisha na kuwapa Ushauri, uelewa mzuri Watanzania lakini kutengeneza bidhaa ambazo zitakidhi na kuleta majibu ya changamoto ambazo Watanzania wanakuwa nazo na watakazo weza kuhimili na kulipia.

Kwa upande wake Francis Kaaya Mkuu wa kitengo cha Bima kutoka Benki ya Biashara Tanzania amesema wateja wengi wa NIC wamenufaika kutokana na mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo, teknolojia na vifaa ambayo yamepelekea watu wengi kulipwa madai yao kwa wakati tofauti na ilivyokuwa awali ambapo ilikuwa mpaka siku saba.

Hivyo, tunaendelea kuwapongeza NIC kwa tuzo ambazo wanazoendelea kuzipata wazitumie kama changamoto waendelee kuja na bidhaa mpya sokoni kwa sababu wao ndio wamelishikilia soko la bima la Tanzania wajitahidi kulipa madai ya wateja kila kukicha na changamoto kubwa ni Elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima ili kuhakikisha wahusika wanapata elimu hiyo.