Na Penina Malundo,Timesmajira
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Bima la taifa( NIC),Kaimu Mkeyege amesema elimu ya bima kwa watanzania bado ipo chini,hivyo jitihada mbalimbali zinatakiwa kufanyika ili watanzania waweze kuelewa umuhimu wa bima hizo kabla ya kusubiri majanga kutokea.
NIC imesema kutokana na upungufu huo wa elimu ya bima kwa watanzania kwa sasa wameamua kuanza kushuka chini,kwa kuwafata wananchi katika maeneo mbalimbali na kuwapa elimu ya bima na umuhimu wake katika maisha ya kila siku.
Akizungumza jana jijini Dar es salaam katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ”Sabasaba”alipotembelea banda hilo,amesema kutokana na watu kuuliza maswali mengi kuhusu umuhimu wa bima na namna unavyosaidia NIC imeona ni vema kuwafata watu katika maeneo mbalimbali na kuwapatia elimu.
“Bima ni jambo zuri hivyo kila mwananchi kwa namna moja au nyingine ni muhimu kuwa na bima katika mali yake yote,kwani inaenda kulinda moja kwa moja mali ya mtu anaimiliki,ila bado elimu ya bima ipo chini kwa watanzania wanavyouliza bima ni nini,”alisema na kuongeza”Wapo wengine hawani umuhimu wa kuwa na bima lakini yanapowakuta ndipo wanaona umuhimu wake,”amesisitiza Mkeyege .
Aidha amesema wanamkakati mkubwa wa kuelimisha jamii lakini pia kutoa mafunzo kwa wanao elimisha jamii kuhusu masuala ya Bima hususan watumishi wao wa NIC kwa kuwawezesha kuongeza uzoefu na ujuzi katika fani yao.
Amesema mafunzo hayo yatakayo tolewa ya muda mfupi mfupi ili waweze kuona namna gani watakavyoweza kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa bima na faida zake endapo mwananachi anapopata majanga.
”Shirika letu ni la Serikali na Shirika la Umma kwa asilimia 100 tunamilikiwa na Serikali tunajukumu kubwa katika kuendeleza kauli mbiu ya mwaka huu ya maonesho ya 48 ya Sabasaba ”Tanzania ni mahali sahihi pa biashara na uwekezaji’.
Mkeyege amesema bima ambazo sio za maisha ndio bima ambazo zinaweza kuhusiana na kauli mbiu hii kwamba uwekezaji unaokuja kuwekezwa nchini unahitaji kukatiwa bima ili pale wawekezaji wanapokuwa wamekwama wanarudishwa katika hali yao ya awali.
”Utakuta mtu kaja kuwekeza nchini,alafu janga linampata kwa namna moja au nyingine wanakuwa wamepoteza fedha zao kutokana na janga lililowapata,ndio maana tunasema bima ni muhimu kwa wawekezaji katika kulinda uwekezaji wao nchini,”amesema.
Pia ameipongeza tantrade kwa uandaaji wa maonesho mazuri mwaka 2024 kwa kuona ni namna gani watanzania walivyoshirika kwa namna moja na nyingine kutembelea mabanda mbalimbali.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato