Na Mwandishi wetu,timesmajira, Online
Shirika la Taifa la Bima (NIC) limeibuka mshindi katika kundi la kampuni za Bima zilizoshiriki katika maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa Sabasaba yaliyohitimishwa Julai 13, 2022.
NIC imepokea kombe la ushindi huo kutoka kwa Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Akizungumza mara baada ya kupokea ushindi huo Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule amesema ushindi huo ni kwa shirika kutokana na kutoa huduma bora kwa wananchi wakati maonesho hayo.
Mwakifulefule amesema kuwa licha ya kuibuka mshindi kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana, kazi yao kubwa ni kuendelea kuwa bora katika kutoa huduma za bima nchini.
Aidha amesema kuwa katika kuonyesha ubora wa huduma kwa wananchi na wadau wa bima kazi kubwa ni kuongeza bidhaa za bima kutokana na mahitaji yaliyopo.
Mkurugenzi huyo amesema wafanyakazi wasibweteke kwa ushindi huo bali kuuendeleza kila panakuwa na ushindani ambao utatokana na kunyesha uwezo wetu katika kutoa huduma za Bima nchini.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba