Na Doreen Aloyce, TimesMajira Online, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 ambayo inatoa unafuu katika maeneo mengi yanayohusu Watanzania, pia kuainisha maeneo mbalimbali ya vipaumbele katika kipindi hicho.
Waziri Mpango alisoma bajeti hiyo jijiji Dodoma jana, huku akiwasilisha mapendekezo mbalimbali ambayo anataka kufanya mabadiliko ikiwemo katika nyanja za sheria na ushuru.
Baadhi ya mapendekezo hayo machache ni kama ifuatavyo;
Mapendekezo ya kuongeza kiwango cha mapato ghafi
Waziri Mpango amependekeza kuongeza kiwango cha Mapato ghafi ya Vyama vya Ushirika vya Msingi yasiyotakiwa kutozwa Kodi ya Mapato kutoka sh. milioni 50 hadi sh.100,000,000 kwa mwaka.
Amesema lengo la hatua hii ni kutoa nafuu ya kulipa Kodi ya Mapato kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi zikiwemo SACCOS kutokana na kuwa na mitaji midogo ili kuwanufaisha wanachama wake kwa njia ya gawio na mikopo.
Pili, amesema anapendekeza kufuta msamaha wa Kodi ya Mapato kwa wazalishaji walio ndani ya maeneo maalum ya kiuchumi wanaozalisha bidhaa na kuuza ndani ya nchi kwa asilimia 100 na kuruhusu michango ya wadau kwenye Mfuko wa Ukimwi isitozwe kodi ya Mapato.
Aidha, amesema anapendekeza michango iliyotolewa na wananchi kwa Serikali na itakayoendelea kutolewa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID 19) isitozwe kodi hadi hapo Serikali itakapotangaza kuisha kwa ugonjwa huu,” amesema na kuongeza;
“Lengo la mabadiliko haya ni kuhamasisha uchangiaji wa hiari katika Mfuko wa UKIMWI na kwa Serikali ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UKIMWI na COVID 19.”
Pia amesema anapendekeza kumpa Mamlaka Waziri wa Fedha kutoa msamaha wa Kodi ya Mapato kwenye miradi ya Kimkakati yenye jumla ya Kodi ya Mapato 75 isiyozidi sh. bilioni moja kwa kipindi chote cha mradi.
Amefafanua kwamba anakusudia kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani ya Mtaji kwenye mapato yatokanayo na ubadilishaji wa leseni (concessional right) katika ardhi iliyohodhiwa (reserved land) na kupangishwa kwa mwekezaji mwingine.
Kwa mujibu wa Waziri Mpango lengo la hatua hiyo ni kupanua wigo wa kodi na kuongeza mapato ya Serikali.
Pia amesema anakusudia kutoza kodi ya zuio ya asilimia 10 kwenye malipo ya uwakala inayolipwa kwa mawakala wa Benki kama ilivyo kwa mawakala wa huduma za uhamishaji fedha za kieletroniki.
Amesema lengo la hatua hii ni kuweka usawa katika utozaji wa kodi ya mapato kwa watoa huduma za kibenki, kielektroniki na huduma za usafirishaji fedha kwa njia ya mitandao ya simu.
Ameongeza kwamba anapendekeza kufanya marekebisho kwenye vifungu vya 3, 4, 6 na 69 vya Sheria ya Kodi ya Mapato ili kuongeza tafsiri ya maneno “beneficial owner”; “representative assessee” na “business connection”.
Lengo la maboresho haya ni kutekeleza matakwa ya nchi kujiunga kwenye Jukwaa la Kimataifa la kubadilishana taarifa za kikodi ili kukabiliana na ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni za kimataifa.
Aidha, amesema maboresho hayo yanalenga kuziba mianya ya ukwepaji kodi ya mapato unaofanywa na makampuni yenye mahusiano mbalimbali ya kibiashara kupitia matawi ya kampuni hizo kwenye nchi mbalimbali.
“Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa ujumla wake zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha sh. bilioni 514.0,” amesema.
Marekebisho ya ushuru wa bidhaa
Pia amesema anapendekeza kufanya marekebisho ya Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zifuatazo;
Kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye bia za unga (powdered beer) zinazotambulika kwa HS Code 2106.90.99 kwa kiwango cha sh. 844 kwa kilo ya bia ya unga inayoagizwa kutoka nje ya nchi.
“Lengo la mabadiliko haya ni kupanua wigo wa kodi kwa kuwa bidhaa hizi kwa sasa zinaagizwa toka nje ya nchi; na pia kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye juisi za unga zinazotambulika kwa HS Code 2106.90.99 kwa kiwango cha sh. 232 kwa kilo ya juisi ya unga inayoagizwa kutoka nje ya nchi.
“Lengo la mabadiliko haya ni kupanua wigo wa kodi kwa kuwa bidhaa hizi kwa sasa zinaagizwa toka nje ya nchi.
Hatua za kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha sh. bilioni 45.8,” amesema Waziri Mpango.
Pia amesema anapendekeza kufanya maboresho kwenye Sheria ya Usimamizi wa Kodi Sura 438, ili kumwezesha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutatua mapingamizi ya kodi kwa ufanisi na haraka.
Marekebisho haya ni pamoja na kuweka ukomo wa muda wa siku 30 za kuwasilisha nyaraka zitakazotumika kwenye utatuzi wa pingamizi.
“Aidha marekebisho haya yataweka ukomo wa miezi sita kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kufanya maamuzi ya mapingamizi ya kodi. Kwa sasa, sheria haitoi ukomo kwa walipakodi kuwasilisha nyaraka zitazoisaidia Mamlaka ya Mapato kufanya uamuzi kuhusu pingamizi.
Vile vile, kwa sasa sheria haitoi muda wa ukomo kwa Kamishna Mkuu kwa Mamlaka ya Mapato kufanya uamuzi kuhusu pingamizi,” amesema.
Mabadiliko ya sheria ya fedha
Pia amesema anapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Fedha za Umma Sura 348 ili kuziongeza Taasisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA); Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA); na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwenye orodha ya taasisi zinazochangia gawio au asilimia 15 ya Mapato ghafi kwenye Mfuko wa Hazina.
Amesema hatua hiyo ya marekebisho ya Sheria ya Fedha za Umma inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha sh. bilioni 5.89.
Amesema anapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Usajili wa Magari Sura 124, ili kuanzisha usajili wa magari kwa kutumia namba maalum (mfano T. 777 DDD) kwa ada ya sh. 500,000. Ili kuwezesha wateja kuchagua namba ya usajili wa gari katika namba zilizopo katika regista ya namba za magari katika muda husika.
“Hatua hizi za marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Magari inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha sh. milioni 200.
Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290
Waziri Mpango amesema napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290, ili kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya masuala yanayohusu Serikali za Mitaa kukusanya tozo ya huduma (Service Levy) ya asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwenye Sekta ya Mawasiliano kwa niaba ya Halmashauri, na kuyagawa mapato hayo kwa Halmashauri zote ndani ya siku 14 baada ya kukusanywa.
Amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI ataandaa kanuni ambazo zitaweka utaratibu wa ukusanyaji na ugawaji wa mapato hayo kwa kutumia kikokotoo maalum kwa kuzingatia kiasi cha Tozo ya Huduma kutoka Sekta ya Mawasiliano kwa kila Halmashauri.
“Hatua hii itasaidia kuziondolea kero baadhi ya Halmashauri ya kukosa mapato kutoka kwenye chanzo hiki na kupunguza usumbufu wa ufuatiliaji wa kila Halmashauri kwenye Makao Makuu ya Makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano nchini,” Dkt. Mpango.

Sheria ya Ardhi, Na. 4 ya Mwaka 1999
Waziri amesema napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Ardhi, Na. 4 ya Mwaka 1999 ili kuweka ulazima wa mwananchi yeyote ambaye ardhi yake imefanyiwa upimaji (survey) na michoro yake kuidhinishwa na Wizara yenye dhamana ya masuala ya ardhi kupeleka maombi kwa Kamishna wa Ardhi kupatiwa hati ya kumiliki ardhi ndani ya siku tisini (90) kuanzia tarehe ya kuidhinishwa kwa michoro ya upimaji.
“Lengo la marekebisho haya ni kuwafanya wananchi wanaohodhi ardhi bila umiliki wafanye taratibu za kuomba umiliki,” amesema.
Wakulima wa ndani
Ili kulinda wakulima wa ndani ili kuendeleza kilimo cha mbogamboga na maua hapa nchini, amesema anapendekeza kuendelea kutoza ushuru wa forodha kwa kiwango cha asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za fito za plastiki zijulikanazo kama PVC Profiles HS Code 3916.10.00; 3916.20.00; 3916.90.00 ambazo hutumika kwa ajili ya kutengenezea fremu za milango, madirisha n.k. Lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali;
Pia kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi zinazozalishwa na kiwanda cha mufindi hapa nchini ambazo zinazotambulika kwa HS codes 4804.11.00; 4804.21.00; 4804.29.00; 4804.31.00 na 4804.41.00.
Lengo la hatua hii ni kuendelea kulinda kiwanda cha mufindi na kuongeza uzalishaji wa karatasi hapa nchini;
“Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 35 kwenye ngano inayotambulika kwa HS Code 1001.99.10 na HS Code 1001.99.90 kwa utaratibu wa “Duty Remission” ambapo wanaonufaika na unafuu huu ni wenye viwanda vya kusaga ngano.
Hatua hii imezingatia makubaliano na Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na kwamba uzalishaji wa ngano katika nchi hizi hautoshelezi mahitaji, na bidhaa hii ni muhimu katika kutengeneza vyakula mbalimbali.
Lengo la Serikali ni kuwezesha Viwanda na walaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa ngano waweze kupata vyakula husika kwa bei nafuu na tulivu,” amesema.
Ameongeza kuwa hatua nyingine ni kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwa utaratibu wa duty remission kwenye bidhaa ijulikanayo kama “Printed Alluminium Barrier Laminates” (ABL) HS Code 3920.10.90 ambayo hutumika kama malighafi ya kutengeneza vifungashio vya dawa ya meno kwenye viwanda vya ndani, kwa mwaka mmoja;
Hatua nyingine ni kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 10 kwa utaratibu wa “Duty Remission” kwenye malighafi ya kutengeneza sabuni ijulikanayo kama RBD Palm Stearin (HS Code 1511.90.40) kwa viwanda vinavyotengeneza sabuni nchini. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa viwanda vya kuzalisha sabuni nchini.
Pia amesema anapendekeza kufuta tozo ya mafunzo ya elimu kwa umma iliyokuwa natozwa kiasi cha sh 250,000 kwa kila mshiriki kwa kuwa hili ni jukumu la msingi la OSHA kuelimisha umma.
Eneo lingine ni kupendekeza kufuta ada ya ukaguzi iliyokuwa inatozwa kwa kiwango cha asilimia 80 ya ada ya usajili, ada hii inaleta mkanganyiko kwa kuwa tozo ya usajili ilishafutwa.
Amesema anapendekeza kupunguza ada ya uchunguzi wa ajali iliyokuwa ikitozwa kiasi cha sh 500,000 kwa kila mtaalamu anayefanya uchunguzi hadi sh 120,000 kwa kila mtaalamu lakini si zaidi ya sh. milioni 1.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja