Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limesaini mkataba wa makubaliano na Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), kwaajili ya uwezeshaji wa utoaji wa mikopo kwa Wafanyakazi wa serikali, sekta binafsi, wakulima na watanzania ili kuweza kumiliki nyumba zilizojengwa na Shirika la nyumba la Taifa hapa Nchini.
Akizungumza leo februari 07, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano na Shirika la Nyumba la Taifa na Benki ya watu wa Zanzibar kwaajili ya kutoa mikopo ya nyumba kwa wateja wa Shirika la Nyumba, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Hamad Abdallah amesema watanzania watakiwa kuchangamkia fursa ili kuweza kumiliki nyumba mapema.
“Sisi katika makubaliano yetu ile hati tutaipeleka kwenye benki na kuna masharti yao awali unatakiwa ulipe nini, ili uweze kuwa na vigezo vya kupatia mkopo kutoka benki ya watu wa Zanzibar, tofauti na zamani ili uchukue mkopo lazima uwe na dhamana nyingine” amesema Mkurugenzi Mkuu wa NHC Hamad Abdallah
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Hamad Abdallah amewapongeza PBZ kwa kuungana na NHC katika kuwawezesha watanzania kumiliki nyumba mapema, pia kwa wanunuzi watarajiwa wa Morocco Square, benki ya PBZ wapo tayari kuwasapoti ili muweze kupata umiliki wa nyumba hizo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Dkt Muhsin Masoud, amesema Benki hiyo kongwe Zanzibar kwa Tanzania bara ina jumla ya matawi kumi ambapo ni Dar es Salaam yapo matawi nane, Dodoma matawi mawili na Mtwara matawi mawili.
Hivyo, matarajio yao makubwa ni kuendelea kuongeza matawi mengi Tanzania bara ili kuendelea kuimarisha na kukuza utoaji wa huduma ya haraka kwa Watanzania wote, Mkurugenzi Mkuu wa (PBZ) Dkt Muhsin Masoud ameongezea kuwa wanatarajia kwa mwaka huu kuongeza matawi mengine kwa mikoa ya Arusha, Mwanza, Morogoro, Tanga na Mbeya.
More Stories
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?
Watendaji Songwe wapatiwa mafunzo uboreshaji daftari la mpiga kura
Samia: Mwaka 2024 ulikuwa wa mafanikio